Home Kitaifa Serikali yatenga milioni 400/- kwa soko la muda Kawe baada ya janga...

Serikali yatenga milioni 400/- kwa soko la muda Kawe baada ya janga la moto

Serikali imesema ujenzi wa soko la muda kwa wafanyabiashara waliokumbwa na janga la moto katika soko la Kawe utakamilika ndani ya wiki mbili, huku kiasi cha shilingi milioni 400 kikiwa tayari kimetengwa kwa ajili hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo Septemba 16,2025 alipofanya ziara katika eneo la Kawe kukagua athari za moto uliotokea alfajiri ya Septemba 15 katika soko la Kawe.

Aidha, Dkt. Jafo aliwahakikishia wafanyabiashara kuwa Serikali inachukua hatua za haraka kurejesha hali ya kawaida ili wafanyabiashara waendelee na shughuli zao za kujipatia kipato wakati Serikali ikiendelea na mipango ya ujenzi wa soko la kudumu.

Mhandisi wa ujenzi kutoka halmashauri ya manispaa lazima ahakikishe kuwa ujenzi wa soko la muda katika viwanja vya Tanganyika Packers unakamilika ndani ya wiki tatu,” amesema Dkt. Jafo wakati wa ziara hiyo.

Vilevile, ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha shughuli za biashara zinaanza tena haraka, huku kukiwa na mpango wa kuwarejesha wafanyabiashara katika soko la kisasa la Kawe mara baada ya ujenzi wa soko la kudumu kupitia Mpango wa pamoja kati ya Serikali na jamii katika kujenga soko jipya na bora zaidi

Dkt Jafo pia alitoa onyo kali dhidi ya kuingilia mchakato wa upangaji wa maeneo katika soko la muda, akisisitiza kuwa hakuna mtu asiyehusika anayepaswa kupewa eneo katika soko hilo la muda.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule alithibitisha kuwa Serikali imetenga shilingi milioni 400/- kwa ajili ya ujenzi wa soko la muda, pamoja na shilingi milioni 100/- za kuwasaidia wafanyabiashara waliopatwa na athari za moto.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi Hanifa Hamza, alisisitiza pia kuwa Serikali kwa itashirikiana na na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) inalenga kujenga soko la kisasa kuchukua nafasi ya lile lililoungua lililopangiliwa vizuri, miundombinu ya Kisasa, uzio na bima dhidi ya majanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!