Home Biashara SERIKALI YAPOKEA CHANGAMOTO ZA WACHIMBAJI WANAWAKE

SERIKALI YAPOKEA CHANGAMOTO ZA WACHIMBAJI WANAWAKE

  • Kuandaa Mkakati wa Uwezeshaji Wanawake
  • Kupewa leseni za maeneo yenye taarifa za Utafiti

Serikali kupitia Wizara ya Madini na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum leo Septemba 29 ,2023 imepokea changamoto zinazowakabili wachimbaji madini wanawake katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama Cha Wachimbaji Wanawake Tanzania ( TAWOMA).

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Mwenyekiti wa TAWOMA Semeni Malale alisema katika kipindi cha miaka 25 TAWOMA imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa leseni za uchimbaji , kutokuwa na vifaa vya uchimbaji , kukosa mitaji pamoja na kutokopesheka katka Taasisi za Fedha.

Semeni alifafanua kuwa TAWOMA inakosa fursa nyingi ndani ya sekta ya madini kutokana nguvu yake ya kiuchumi kuwa ndogo katika mnyororo mzima wa madini.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa Serikali inatambua changamoto zenu hivyo kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) litakabidhi mitambo 5 mitano kwa wachimbaji wadogo kwa ajili ya uchorongaji itakayowasaidia katika kufanya utafiti wa kina ili waweze kuchimbaji kwa uhakika.

Sambamba na hapo Mhe. Mavunde aliongeza kuwa kupitia VISION 2030 wa Madini ni Maisha na Utajiri, upo mpango wa kuwapatia leseni zitakazotolewa katika vikundi vya watu 20 ambapo 15 zitatolewa pindi STAMICO itakapomaliza kuandaa utaratibu.

Kwa upande wake Dkt .Dorothy Gwajima Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsi, Wanawake na Makundi Maalum amesema Serikali ya Awamu ya Sita inatoa nafasi kubwa kwa wanawake hususani katika Sekta za Uchumi , hivyo kupitia vyama vya wachimbaji madini wanawake kama vile TAWOMA imepanga kuwajengea uwezo kwa kuwakutanishi na Taasisi za fedha ili kujadiliana namna bora ya kupata mikopo yenye riba nafuu kwa shughuli za uchimbaji madini.

Aidha , akielezea kuhusu mafanikio Malale amesema mpaka sasa TAWOMA imefanikiwa kuratibu mafunzo mbalimbali kwa wanachama ndani na nje ya nchi yanayohusu Afya,Usaamizi mahala pa kazi , utunzaji mazingira katika uchimbaji ,uongezaji thamani madini na biashara ya rasilimali madini.

TAWOMA ilianzishwa mwaka 1997 mpaka sasa ina wanachama zaidi 4000 katika mikoa 21 ikiwa na lengo la kufikia Mikoa yote na kufikisha wanachama zaidi 10000 ifikapo mwaka 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!