Home Kitaifa SERIKALI KUWEZESHA USHIRIKI WA VIJANA KATIKA MAENDELEO YA TAIFA

SERIKALI KUWEZESHA USHIRIKI WA VIJANA KATIKA MAENDELEO YA TAIFA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuweka mifumo imara ya kitaasisi na kisheria itakayowapa vijana fursa pana ya kushiriki na kushirikishwa katika michakato yote ya maendeleo hapa nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiangalia sehemu ya bidhaa za wadau wa masuala ya Vijana walioshiriki kwenye  kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”

Amefafanua kuwa Dhana ya Ushiriki wa Vijana katika kujenga uchumi imara, ustawi na maendeleo endelevu inatokana na kuwa vijana ndio nguvu kazi, vijana ni kundi kubwa ukilinganisha makundi mengine ya kijamii, vijana ni wabunifu, vijana ni wavumbuzi na vijana ni wadadisi.

Baadhi ya Vijana wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”

Mhe. Ndalichako ameyasema hayo leo tarehe 12 Agosti, 2022, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”.

“Vijana ni watu wenye mawazo mapya, Vijana ndio chachu ya mabadiliko yenye tija ya Kisayansi na Kiteknolojia na Vijana ndio warithi na waendelezaji wa historia na falsafa ya Mataifa yao.”

Baadhi ya Vijana wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”

Mhe. Ndalichako amesisitiza kuwa kiwango cha ushiriki wa vijana kwenye shughuli za kiuchumi na za kijamii kwa ajili ya ujenzi wa Taifa hapa nchini kipo kwa 80%.

“Matokeo ya utafiti wa nguvu kazi ya Taifa ya Mwaka 2020/21 yanaonesha kuwa, idadi ya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 inakadiriwa kufikia watu Milioni 18.3. Kati yao, vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwa maana ya economically active population ni Milioni 14.6.”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo  katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa kati ya watu Bilioni 8 Duniani kote, Idadi ya Vijana ni Bilioni 1.8.

Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu imeratibu Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, Vijana Tanzania Bara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walitekeleza masuala mbali mabli kama vile; Kongamano la Kitaifa na shughuli za kujitolea kwenye usafi wa mazingira katika fukwe za bahari na Bonanza la Michezo.

Wazo la kuwa na Siku ya Vijana Kimataifa lilitolewa na vijana kwenye Mkutano wa Vijana wa Dunia (World Youth Forum) uliofanyika Mjini Vienna nchini Australia Mwaka 1991. Kuanzia tarehe 12 Agosti, 2000 nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa, ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!