Home Kitaifa SEKTA YA MADINI IMEINUA WATU WENGI KIUCHUMI

SEKTA YA MADINI IMEINUA WATU WENGI KIUCHUMI

Na Magrethy Katengu–Dar es salaam

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Sekta ya madini ni nguzo muhimu katika uchumi wa Nchi, hivyo serikali itaendelea kuifungamanisha na sekta nyingine ikiwemo sekta ya viwanda kwa kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza katika viwanda na hatimaye kukuza uchumi na kuleta Maendeleo.

Majaliwa ameyasema hayo Jijini Dar es salaam Novemba 19,2024 wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika Mkutano huo mkubwa wa kimataifa unawakutanisha wadau wa madini wanaojishughulisha na utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani madini, wasimamizi wa Sekta kutoka Serikalini, watoa huduma migodini na wafanyabiashara na kauli mbiu yake mwaka huu ni “Uongezaji wa Thamani ya Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi”uliofanyika katika Ukumbi wa Julius Kambarage Nyerere

Amesema serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuweza kusaidia shughuli za uongezaji thamani madini inaendelea kufanyika hapa nchini.

“Sekta ya madini nchini imekuwa hivyo serikali inaendelea kuboresha mazingira kwa wachimbaji wadogo ili ifikapo 2030 wachimbaji hao wawe wachimbaji wa kati ili waendelee kuchochea uchumi na kuchangia kwenye pato la taifa,” amesema.

Ameongeza kuwa wizara ya madini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeendelea kufanya Utafiti katika maeneo mbalimbali nchini ili kubaini fursa za uwepo wa Madini yatakayotumika kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa mbolea katika sekta ya KILIMO na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo za urembo.

Aidha Majaliwa ametoa wito kwa m
wadau wa sekta ya madini kuhakikisha wanatumia Teknolojia rafiki kwa Mazingira ili kuhakikisha sekta hiyo inakuwa sehemu ya juhudi za mapambano ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na si kuchangia uharibifu wa Mazingira.

Pia ameagiza idara ya Mazingira kushirikiana na wizara ya madini ili kuhakikisha shughuli zote za uchimbaji madini haziathiri Mazingi

“Tanzania inamadini muhimu yanayochimbwa katika maeneo mbalimbali hivyo suala la utunzaji Mazingira ni lazima lizingatiwe. Hivyo wadau wote wa sekta ya madini Wana wajibu wa kuzingatia miongozo ya Mazingira katika utekelezaji wa shughuli za uchimbaji madini ili kulinda Mazingira,” amesisisitiza.

Awali Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema mafanikio katika sekta ya madini yametokana na uongozi bora wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwajali wachimbaji wote wadogo, wakati na wakubwa lakini pia kuongeza bajeti kutoka bilioni 89 mpaka bilioni 231.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawajali sana wachimbaji na ameelekeza mashine mbili za uchorongaji zipelekwe kwa wakinamama wachimbaji,” amesema Mavunde.

Amesema Serikali tayari imeshatunga sera ya kuongeza thamani madini ili kusaidia vijana wengi nchini kupata ajira lakini pia kukuza na kuongeza pato la Taifa.

Katika hatua nyingine KAMPUNI ya dhahabu ya Barrick inayoendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals, imetunikiwa tuzo ya udhamini mkuu wa mkutano wa uwekezaji katika sekta ya Madini na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt.Samia Suluhu Hassan, baada ya ufunguzi wa mkutano huo

Akiongea katika mkutano huo kabla ya kukabidhiwa tuzo hizo,Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido, amewaeleza wajumbe wa mkutano huo jinsi ubia wa Barrick na Twiga unavyoendelea kupata mafanikio makubwa na kuwa mfano wa kimataifa unaodhihirisha kuwa Serikali inaweza kushirikiana na sekta binafsi na kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi.

Ngido, ameeleza kuwa katika kipindi kifupi kupitia ubia huu, umeweza kuchangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa kupitia kodi na tozo mbalimbali za Serikali, kuongeza ajira kwa watanzania, kufanikisha miradi mikubwa ya kijamii hususani katika sekta ya barabara, afya, maji, na elimu pia umefanikisha kuinua uchumi wa wazabuni wa kitanzania wanaouza bidhaa mbalimbali kwenye migodi yake ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!