
Na Boniface Gideon
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Batilda Burihani , tarehe 27 ameongoza wananchi katika zoezi la kupiga kura la uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo wanachagua viongozi wa Serikali ya Mtaa, kitongoji na vijiji katika Mkoani Tanga.
Akizungumza baada ya kupiga kura, Mhe. Batilda aliwashukuru wananchi wa Mkoa wa Tanga kwa ukomavu wao wa kisiasa na kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo, akieleza kuwa ni ishara ya maendeleo katika demokrasia. Aliwataka wananchi kuendelea kushiriki kwa wingi ili kuchagua viongozi wanaowataka, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo linatakiwa kuwa la amani na utulivu.
“Tunashuhudia ukomavu mkubwa wa kisiasa kutoka kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga Kampeni zilifanyika kwa amani na hakuna malalamiko kutoka kwa vyama au wagombea,” alisema Mhe. Batilda “Ninawaomba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wanachagua viongozi bora watakaowaongoza katika maendeleo ya jamii yetu.”
Mhe. Batilda pia aliwasisitizia vyama vya siasa na wanachama wao kuheshimu kanuni za uchaguzi, akieleza kuwa malalamiko yoyote kuhusu uchaguzi yanapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi.
Aidha, Mhe. Batilda aliwataka wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima wakati wa uchaguzi, akiwataka waendelee na shughuli zao baada ya kupiga kura, ili kuepuka msongamano na usumbufu. na Alisisitiza kuwa hii ni siku ya mapumziko iliyotengwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili wananchi waweze kushiriki kwa wingi katika uchaguzi.pia uchanguzi huu unatupa taswira ya uchanguzi ujao Madiwani,wabunge,na ngazi ya Rais.