Home Kitaifa NLD YAZINDUA RASMI KAMPENI UCHAGUZI S/MITAA,KIKILAANI WANUFAIKA TASAF KUFANYISHWA KAZI NGUMU,AAHIDI KULIPIA...

NLD YAZINDUA RASMI KAMPENI UCHAGUZI S/MITAA,KIKILAANI WANUFAIKA TASAF KUFANYISHWA KAZI NGUMU,AAHIDI KULIPIA 30000 KILA MZEE.

Na Boniface Gideon, HANDENI

CHAMA cha The Nation League For Democracy (NLD) hatimaye kimezindua rasmi kampeni zake kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu, huku kikija na agenda lukuki ambazo zitasaidia kuongeza wigo wa ajira na Maendeleo Nchini,na kulaani vikali Serikali kuwatumikisha kazi ngumu ikiwemo kuchimba mitaro,visima na mabwawa kwa Wanachama wa TASAF.

Uzinduzi wa kampeni zake zimefanyika katika Kijijij cha Kwedikwazu wilayani Handeni,ambapo chama hicho kimesimamisha wagombea kwa sehemu kubwa ya Vijiji na mitaa Wilayani humo,
Akizungumza na Wakazi wa Wilaya hiyo,Katibu Mkuu wa NLD Doyo Hassan Doyo amesema,chama hicho kimesimamisha wagombea kwenye mitaa na vijiji zaidi ya 700 n nchini na kinatarajia kupata ushindi katika maeneo yote yenye Wagombea,

“Chama chetu kimesimamisha wagombea kwenye mitaa na vijiji vingi nchini,kwa kwa Kijiji hiki tumesimamisha wagombea kwenye mitaa yote na wajumbe,pia Wilaya yetu tumesimamisha wagombea kwenye mitaa na vijiji karibu maeneo yote,tunatarajia kuchukua ushindi katika maeneo yote yenye Wagombea wetu,kwani tumesimamisha wagombea wanaokubalika katika jamii na wenye sifa njema na mfano wa kuigwa katika jamii,hivyo hatuoni sababu yakutokushinda” Alisisitiza Doyo Hassan Doyo

Doyo alisema katika Kijijiji hicho cha Kwedikwazu,kinategemewa kwa uzalishaji wa madini lakini kwenye account ya Kijiji hicho hakuna hata mia Mbovu,
” Kijiji hiki kina madini lakini kwenye account ya Kijiji hakuna hata mia Mbovu,mana yake uongozi uliokuwepo madarakani umeshindwa kusimamia maslahi ya Wakazi wa Kijiji hiki,sisi NLD tukiingia madarakani tutahakikisha Kijijiji hiki kinapata mapato kutokana na madini ,tutajenga ofisi nzuri ya Kijiji pamoja na Madarasa mazuri yakusomea”Alisisitiza Doyo Hassan Doyo

Kuhusu kutumikishwa kazi ngumu kwa wanufaika wa TASAF,Doyo alisema, Serikali imekuwa na tabia yakuwatumikisha Wanachama wa TASAF kufanya kazi ngumu na kuahidi yupo tayari kuwalipia kila Mzee Sh.30,000 kila mwezi bila kufanya kazi ngumu,
“Serikali yetu imekuwa ikiwatumikisha kazi ngumu wazee wanaopata fedha za TASAF,wanachimba mabwawa,kuchimba mitaro, visima nk, lakini pia kwenye Wanachama wa TASAF wamo vijana Wenye umri mdogo,kitu ambacho ni kinyume na malengo ya mpango wa TASAF, lengo la TASAF nikusaidia Kaya Maskini hususani wazee, lakini wazee hao ndo wanatumikishwa kazi ngumu,nipo tayari kuwalipia elfu 30 kila mwezi kwakila Mzee katika Kijijiji hiki endapo tutashinda Uenyekiti”Aliongeza Doyo Hassan Doyo

                MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!