Home Michezo NGUMI ZIPO MABIBO NA MAZENSE, TEMEKE WABAKI NA UKONGWE

NGUMI ZIPO MABIBO NA MAZENSE, TEMEKE WABAKI NA UKONGWE

Bondia wa Ngumi za Kulipwa Jackson Malinyingi amemjibu Mpinzani wake Peter Toshi wa Temeke akiahidi kumpiga kama Begi kwenye Pambano la Dar Boxing Derby litakalopigwa Novemba 20,2022, Kinesi Dar es salaam. 

Akizungumza wakati akiendelea na mazoezi yake City Center Gym iliyoko mabibo Jijini Dar es Salaam Jackson Malinyingi amesema yeye sio Daraja la kila Bondia kuvuka hivyo mpinzani wake atapokea kipigo ambacho hajawai kupata kwenye Mchezo Wa ngumi. 

Mpinzani wangu ajitahidi kufanya mazoezi ajiandae mnyama mkali nakuja atapata kipigo kikali.”

Kwa Upande wa wadau wa Masumbwi Kutoka Mabibo wamesema Kwa sasa Temeke hakuna Ngumi Huku wakijinasibu kuwa Mafundi Wa mchezo wa Masumbwi wanatokea Manzese na Mabibo.

Mkufunzi Wa Bondia huyo kocha Hamad Andrea Kiungo amesema Ngumi Mazoezi na sio Imani za Kishirikina hivyo Watoto wa Temeke Wajiandae Kwa Kipigo Kwenye Pambano Hilo La Dar Boxing Derby.

Mabondia Wengine watakao panda Ulingoni Kwenye Pambano la Dar Boxing Derby Lenye Lengo La kupata vipaji Vipya Bondia Paul Magensta na Haruna Ndaro,Hamad Furahisha na Max Mushi, Dick Zombie na Sylvester Urio huku Roja MJESHI akizichapa na  SAIDI Macho katika Uwanja Wa Kinesi Novemba 20,2022 Dar es salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!