
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha ndani ya miezi sita inatengeneza na kukamilisha sera ambayo itajumuisha vitu vingi ambayo itaongoza Biashara bunifu (Startups) ili kuratibu kwa kushirikiana na sekta nyingine zenye biashara bunifu mbalimbali.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Wiki ya Biashara Bunifu Tanzania 2026 (Tanzania Startup week 2026) uliofanyika Oktoba 19,2026 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Ndejembi ameingeza kuwa mpango wa Serikali ya awamu ya sita ni kutengeneza kituo kikubwa kwa ajili ya Startup kukutana na kuendeleza mawazo yao , hivyo ameiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Viwanda na Biashara kuratibu na kutafuta jengo maalum ambalo litakuwa ni makutano ya startup ili kukuza mawazo hayo.
Aidha amesema Serikali inaiona Biashara bunifu kama eneo linalokua kwa kasi zaidi hivyo inaendelea kusirikiana na kuwashika mkono na kuwajengea mazingira rafiki wamilki wa biashara changa ili kukuza vipaji na mawazo waliyonayo.

Kwa upande wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (Mb) amesema Wizara hiyo imeendelea kuwa kinara katika kuwawezesha na kuwa sehemu ya kusaidia biashara bunifu ambalpo Wizara imeweka katika bajeti ya wizara 2026/2027 kipengele namba 7 pamoja na kuanzisha kitengo cha intelijensia ya masoko ambacho kinaenda sambamba na biashara bunifu.
Aidha Waziri Kapinga ameongeza kuwa Wizara na Taasisi zake zimekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana wabunifu hasa wanaoanza biashara n wafanyabiashara wote nchini kwa urahisi kwani taasisi zimeweka mifumo rafiki ili kupatikana kwa urahisi.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa taasisi ya kukuza biashara bunifu Bwana Zahoro Muhaji amemshukuru Makamu wa Rais kwa kutambua mchango wa taasisi bunifu na kuona umuhimu wa kutambua makampuni hayo kwani ndio vijana watakaokuwa nguvu kazi ya kesho
Kongamano linaambatana na maonesho ya wabunifu mbalimbali kwenye sekta mbalimbali ambao anatoa mchango mkubwa kwenye sekta ya Mawasiliano, Viwanda na Biashara Nishati na nyinginezo.









