Na Magrethy Katengu
Wtanzania wameshauriwa kuwa na Imani na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwani ana maoni makubwa na Nchi hii hivyo waendelee Kumwombea Mungu ambariki amjalie Hekima, Busara katika uongozi wake kuleta Uchumi ulio Imara.
Ushauri huo imetolewa Jijini Dar es salaam na Nabii Mtume wa Kanisa la Bwana Yesu kwa Mataifa yote Philibert Paschal amesema katika maombi yake ya kila siku alionyeshwa kuwa kati ya Rais Dkt Samia anamaono makubwa ya nchi ya Tanzania kwani amefungua Uchumi na anaendelea kuweka mashirikiano Kimataifa Ili Wawekezaji waendeleee kumiminika na vijana wapate ajira.

“Dkt Rais Samia Suluhu analiongoza Taifa vizuri sana na Mimi Nabii kiongozi wa dini nimefanya maombi Maalumu kumuomba Mungu anioneshe maono juu yake ndipo Mungu alinionyesha ni Mwanamke alimjalia hekima Busara aliongoze Taifa na kudumusha Amani iliyoachwa na Waasisi wa Taifa hili hivyo ni vywema kila Mmoja wetu kumwombea” amesema Nabii
Sanjari na hayo amesema wale wote wanaoilalamikia Serikali kuhusu Mfumko wa bei za bidhaa hasa za vyakula waangalie hali ya hewa ya Mwaka 2021 ilibadilika wakulima walilima na hawakupata Sanaa hivyo mavuno yakawa machache hivyo lazima bei zipande lazima Wananchi watambue wasilalamike Wamwombe Mungu Mwaka huu 2022 hali ya hewa ibadilike Ili bei za bidhaa zishuke bei.
Aidha Nabii Philibert ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kumwomba kila mtu kwa Imani yake kuamini kuwa yeye ni mweza wa yote Mwaka huu ataubadilisha utakuwa wa Neema na Baraka mavuno yatakuwa mengi na bei zitashuka








