Home Michezo MSAMA PROMOTION WARUDI KWA KISHINDO, WAIMBAJI NGULI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI KUKUTANA TAIFA

MSAMA PROMOTION WARUDI KWA KISHINDO, WAIMBAJI NGULI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI KUKUTANA TAIFA

Na Magreth Mbinga

MKURUGENZI wa Msama Promotion Alex Msama ametambulisha waimbaji kadhaa waliothibitisha kushiriki katika tamasha la pasaka litakalofanyika Aprili 9 mwaka huu Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 24, 2023 amewataja waimbaji hao kuwa ni Joshua Ngoma kutoka Rwanda, Tumaini Akilimali kutoka Kenya na Zabroni Singers kutoka Tanzania.

Wengine ni Upendo Nkone kutoka Tanzania, Masi Masilia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ambwene Mwasongwe kutoka Tanzania na Joshua Mlelwa kutoka Tanzania.

“Kwasasa tunafanya mazungumzo na waimbaji kutoka Afrika Kusini, Uingereza na Marekani ili kuleta utofauti na matamasha yaliyopiya tunaposema tumerudi kwa kishindo tunamaanisha, amesema Msama.

Pia Msama ameeleza kuwa Tamasha hilo litakuwa zuri na kubwa la kimataifa na la kihistoria ikizingatiwa halijafanyika kwa takribani miaka saba iliyopita.

Aidha tamasha hilo litakuwa na waimbaji wengi, nguli, wakubwa na wakihistoria, hivyo amewataka Watanzania kujiandaa na tamasha hilo ili kupata burudani na kuliombea Taifa la Tanzania dhidi ya majanga ambayo yanaikumba Dunia kwa sasa.

Aidha Msama ameeleza kuwa watatumia tamasha hilo kueleza mazuri yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika miaka miwili ya utawala wake.

Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Emmanuel Mabisa amesema kwa mwaka huu wamejipanga vizuri kwenye suala la muziki.

“Tumeshapata kampuni itakayofunga vifaa vya muziki vya kisasa,” amesema Mabisa.
Amesisitiza kwamba watafanya tamasha kubwa na lakihistoria huku wakisherehekea miaka miwili ya Rais Dkt. Samia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!