
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu, amesema kuwa Wizara ya Nishati itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati nchini ili kuhakikisha nchi inakuwa na uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme, mafuta, na gesi.
Akifungua Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati Machi 22, 2025, Kazungu amesema kuwa Wizara itaendelea kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji, na usambazaji wa umeme, ikiwa ni pamoja na kufikisha Gridi ya Taifa katika mikoa iliyosalia ya Rukwa, Kagera, Lindi, na Mtwara.

Aidha, amebainisha kuwa Wizara itaendelea kutekeleza Mpango wa Taifa wa Nishati wa mwaka 2025 hadi 2030 kwa lengo la kuongeza upatikanaji na uunganishaji wa umeme kwa wananchi, kuongeza mchango wa nishati jadilifu katika uzalishaji wa umeme, kushirikiana na mashirika binafsi katika maendeleo ya sekta ya nishati, na kuhakikisha upatikanaji wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii
