Home Kitaifa BASHUNGWA: WABADHILIFU NA WAZEMBE KWENYE HALMASHAURI ZOTE KUCHUKULIWA HATUA

BASHUNGWA: WABADHILIFU NA WAZEMBE KWENYE HALMASHAURI ZOTE KUCHUKULIWA HATUA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martin Shigela kuwachukulia hatua wote waliotajwa na timu maalumu iliyochunguza mifumo ya ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya Kilosa.
 
Pia amewaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kutekeleza maelekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) na kuwashughulikia waliotajwa kwenye ripoti katika muda uliotolewa 
 
Bashungwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kilosa baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi iliyofanywa katika Halmashauri hiyo mwezi Machi,2022.


 
Amesema “Si wakati sasa wa kubebana wala kuoneana aibu, hatumtendei haki Rais wetu Samia Suluhu Hassan, pale inapokuja miradi wanatokea watu wachache wanaenda tofauti na taratibu za utumishi wa umma, ninachotaka sasa kila Mkuu wa Mkoa achukue hatua kwenye eneo lake.
 
Sisi watumishi wa umma tulioaminiwa na watanzania kuwa ndani ya Serikali lazima tuendelee kuwa waaminifu, waadilifu na maelekezo hayo Mheshimwa Rais amekuwa akiyasema mara nyingi. Kwa watumishi ambao mko TAMISEMI tutaendelea kuchukua hatua bila kuchoka mpaka tutakapobadilika.”
 
Alisema taarifa ya timu maalum ya uchunguzi uliofanyika kilosa imebaini kuwepo matumizi mabaya ya mashine za kieletroniki za ukusanyaji mapato (POS) huku baadhi ya watumishi wakishirikiana na wakusanya mapato kuhujumu mashine hizi.

” Kwa madudu yaliyobainika hapa Mwenyekiti wa Halmashauri, Baraza la Madiwani na Kamati ya Fedha na uongozi inabidi kubadilika, na hii ni kwa Kamati za fedha na uongozi ndani ya halmashauri zetu zote zinapaswa kujitafakari.”


Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Shigela amesema atatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Bashungwa kuhusu Kilosa pia kama Mkoa wamewekwa mkakati wa kudhibiti mianya ya upotevu mapato, kutozalisha madeni mapya na kuwabainisha wanaodaiwa miaka ya nyuma ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!