
Mjasiriamali na mfugaji wa kuku kutoka Mapinga, Bagamoyo, Raphael Emmanuel, amejishindia pikipiki kupitia promosheni iliyoandaliwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya PigaBet.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi hiyo iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Raphael amesema ushindi huo utamsaidia kurahisisha shughuli zake za kila siku, hususan usafiri.

Amesema kabla ya kupata ushindi huo alikuwa anakabiliwa na changamoto ya gharama kubwa za usafiri, hali iliyokuwa ikiathiri ufanisi wa shughuli zake za kiuchumi.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa kampuni hiyo, Hemed Msonge, amesema promosheni hiyo inahusisha utoaji wa pikipiki mbili kila wiki kwa kipindi cha wiki sita mfululizo, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kampuni hiyo kwa wateja wake.
Ameongeza kuwa droo za promosheni hiyo zinaendelea kufanyika kila wiki hadi kukamilika kwa kampeni hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa washiriki kuzingatia kanuni za uwajibikaji wanaposhiriki michezo ya kubashiri.








