Home Kitaifa MCHENGERWA AWAFUNDA VIONGOZI WAPYA WA UDART, DART

MCHENGERWA AWAFUNDA VIONGOZI WAPYA WA UDART, DART

Na John Mapepele

Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa leo amekutana na viongozi wapya wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na kuwataka kutatua mara moja changamoto ya usafiri wa jiji la Dar es Salaam na kuifanya historia.

Viongozi hao wapya walioteuliwa hivi Karibuni na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan waliohudhuria kikao hicho kilichoitishwa na Waziri Mchengerwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya DART, David Kafulila na UDART, Balozi, Dkt. Ramadhan Dau na Watendaji Wakuu wa taasisi hizo.

Mhe. Waziri Mchengerwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Adorf Ndunguru na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Sospita Mtwale ambapo amesema dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wanapata huduma bora.

Ndugu zangu nendeni mkafanye kazi kwa weledi na kuondoa kabisa changamoto ya usafiri kwa wananchi wetu, hakuna sababu yoyote kwa sasa kuendelea na changamoto hiyo wakati Serikali imeshafanya mapinduzi makubwa kwenye suala la miundombinu na usafiri kwa ujumla katika jiji la Dar es Salaam“. Amefafanua Mhe. Mchengerwa

Amesema baada ya kuboresha huduma hii katika jiji la Dar es Salaam, Serikali itaendelea kupanua katika maeneo mengine nchini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) Balozi Dkt. Ramadhani Kitwana Dau amemhakikishia Mhe. Mchengerwa kuwa viongozi wa UDART na DART wanakwenda kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta mapinduzi makubwa katika kuondoa kabisa changamoto ya usafiri.

Mheshimiwa Waziri kwa niaba ya wenzangu naomba nitumie nafasi hii kukuhakikishia kwamba katika kipindi kifupi tunakwenda kutekeleza maelekezo yako ya kuboresha huduma, lakini pia tunaomba utufikishie salamu za shukrani kwa Mhe. Rais kwa imani aliyotupatia ya kututeua katika nafasi hizi. Tunaahidi hatutamwangusha“. amesisitiza Balozi Dau.

Aidha, amefafanua kuwa hakuna sababu kwa UDART kupata harasa endapo kutakuwa na usimamizi madhubuti na kusisitiza kwamba uongozi wa sasa utakwenda kusimamia kikamilifu ili kutimiza ndoto za mheshimiwa Rais.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!