Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO ” APOI”AENDELEA KUWATAFUTIA KURA WENYEVITI WA MITAA CCM

MBUNGE MATHAYO ” APOI”AENDELEA KUWATAFUTIA KURA WENYEVITI WA MITAA CCM

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo ” apoi” akiendelea kulizunguka jimbo la Musoma mjini kuwatafutia kura Wenyeviti na wajumbe kutoka Chama cha Mapinduzi.

Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 20 mbunge huyo kwa kushirikiana na viongozi wa CCM wamekuwa wakipita kwenye mitaa kuwatafutia kura wagombea hao.

Leo novemba 25 mbunge huyo atanzuguka kwenye mitaa ya Makoko,Mwisenge na Nyasho katika muendelezo wa kutafuta kura za wagombea hao.

Akizungumza na MZAWA BLOG kuhusu mwenendo wa kampeni hizo mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema anauona ushindi wa wagombea wa CCM kwa kuwa wamesimamisha wagombea safi na wanao kubalika.

Amesema kila alupipita kuomba kura kwenye mitaa mbalimbali wananchi wamemuakikishia kuwachagua wagombea hao.

” Kwa muda mfupi wa kampeni nimepita mitaa mbalimbali kuwaombea kura wagombea wa CCM na wananchi wameahidi kutuchagua.

” Niwahakikishie wananchi mitaa yote 73 ya jimbo la Musoma mjini tumesimamisha wagombea safi wawaamini na kuwachagua”,amesema.

Mathayo amesema wagombea wanaotokana na Chama cha Mapinduzi wamechujwa na kupikwa kupitia vikao na kujilidhisha wana uwezo wa kuingoza na kuwaletea maendelei wananchi.

Uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika novemba 27 kote nchini mikoa ya Tanzania bara ukishirikisha vyama 19 vyenye usajili nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!