KATIBU Tawala Msaidizi Sehemu ya Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Dodoma Bi.Mwajabu Nyamkomora,akizungumza wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Baraza la Ushindani (FCT) kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Mzalendo blog -DODOMA
KATIBU Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma, Mwajabu Nyamkomora, amesema uwajibikaji na uaminifu ni miongoni mwa misingi muhimu inayochochea biashara endelevu na kukuza uchumi wa wananchi.
Bi.Nyamkomora ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara kuhusu shughuli za Baraza la Ushindani (FCT) kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma.
Amesisitiza kuwa wadau wa biashara wanapaswa kuzingatia maadili hayo ili kujenga mazingira bora ya ushindani wa haki sokoni, hatua itakayoongeza imani kwa wawekezaji na kuimarisha ustawi wa uchumi.
“Biashara endelevu inahitaji uwajibikaji na uaminifu. Bila misingi hiyo, ni vigumu kujenga soko lenye ushindani wa haki na linalomnufaisha mlaji,” amesema Bi. Nyamkomora.
Aidha ameeleza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa wa wadau kuhusu majukumu ya Baraza hilo pamoja na namna ya kulifikia kwa urahisi wanapokumbana na changamoto za kibiashara.
Kwa mujibu wake, elimu hiyo itawasaidia washiriki kutambua njia sahihi za kutatua migogoro inayohusiana na ushindani wa kibiashara na masuala ya udhibiti wa soko, jambo litakalosaidia kuimarisha biashara na kuongeza ufanisi katika shughuli za kiuchumi.
“Kupitia semina hii, kama sekta na wadau wetu muhimu tunaendelea kuimarisha mshikamano, kubadilishana uzoefu na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu,” ameongeza.
Hata hivyo amewataka wadau kujikita katika misingi ya uwajibikaji na uaminifu ili kuvutia uwekezaji unaoendana na kasi ya maendeleo ya Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Bi.Nyamkomora amebainisha kuwa Ofisi ya Mkoa itaendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Baraza la Ushindani kwa kutoa ushirikiano wa kutosha utakaowezesha utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo, kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na kukuza ustawi wa wananchi.
Kwa upande wake, Msajili wa Baraza la Ushindani, Mbegu Kaskasi, amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Baraza kutoa elimu kwa wadau kufuatia maelekezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, ya kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya taasisi hiyo.
Naye Mkuu wa Idara ya Uchumi wa FCT, Kulwa Msogoti, ameeleza kuwa Baraza hilo ni chombo cha kisheria kinachosikiliza rufaa za ushindani na kulinda maslahi ya wafanyabiashara pamoja na watumiaji wa bidhaa na huduma, kwa lengo la kujenga uchumi shindani na jumuishi nchini.
Nao Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema kuwa mafunzo hayo yamewapa mwanga kuhusu namna ya kufuata taratibu sahihi za kisheria wanapokumbana na changamoto za ushindani au wanaporidhika na maamuzi ya mamlaka za udhibiti.
Semina hiyo ni sehemu ya mkakati wa Baraza la Ushindani wa kuwafikia wadau katika mikoa mbalimbali nchini ili kuongeza uelewa wa sheria za ushindani na kuimarisha utatuzi wa migogoro kwa njia ya kisheria.

KATIBU Tawala Msaidizi Sehemu ya Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Dodoma Bi. Mwajabu Nyamkomora,akizungumza wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Baraza la Ushindani (FCT) kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma.

MSAJILI wa Baraza la Ushindani (FCT), Mbegu Kaskasi,akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Baraza la Ushindani (FCT) kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Dodoma Bi. Mwajabu Nyamkomora (hayupo pichani) wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Baraza la Ushindani (FCT) kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma.

MKUU wa Idara ya Uchumi FC Bw.Kulwa Msogoti,akiwasilisha mada wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Baraza la Ushindani (FCT) Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma.

MKUU wa Idara ya Sheria FCT Bw.Kunda Mkenda,akiwasilisha mada kuhusu Sheria wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Baraza la Ushindani (FCT) Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma.

AFISA TEHAMA FCT Athuman Kanyegezi,akiwasilisha mada kuhusu TEHAMA wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Baraza la Ushindani (FCT) Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma.

WADAU mbalimbali wakichangia mada na kutoa ushauri wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Baraza la Ushindani (FCT) Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma.

KATIBU Tawala Msaidizi Sehemu ya Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Dodoma Bi. Mwajabu Nyamkomora,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Baraza la Ushindani (FCT) kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 27,2026 jijini Dodoma .