Home Kitaifa DKT. SAMIA AHAHIDI UMEME WA UHAKIKA TABORA

DKT. SAMIA AHAHIDI UMEME WA UHAKIKA TABORA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Septemba 12, 2025 akiwa Tabora Mjini Mkoani Tabora, ameahidi kumaliza changamoto ya kukosekana kwa umeme wa uhakika Mkoani humo ili kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara Mkoani humo pamoja na uhaba wa umeme kwenye baadhi ya maeneo Mkoani humo.

Dkt. Samia wakati wa Mkutano wake wa Kampeni kwenye siku ya pili na ya mwisho Mkoani humo amesisitiza pia kujenga kituo kingine cha kupokea, kupooza na kudhibiti usambazaji wa umeme kwenye eneo la Zimba Wilayani Igunga Mkoani humo kama sehemu pia ya kusaidia katika udhibiti wa umeme.

Kituo cha Zimba kitakuwa kituo cha pili kujengwa Mkoani humo mara baada ya kujengwa kwa kituo kingine kinachohudumia Wilaya za Urambo na Kaliua, suala ambalo limesaidia katika udhibiti wa umeme kwenye Wilaya hizo.

Katika hotuba yake Mgombea huyo wa Urais ameeleza pia kuhusu utekelezaji wa ahadi yake ya upanuzi wa uwanja wa ndege Tabora, akisema kiwanja hicho kimeboreshwa na kupanuliwa na sasa uwanja huo una uwezo wa kuhudumia ndege kubwa zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!