Home Kitaifa Dkt. Jafo Aahidi Zahanati Kila Kijiji Kisarawe

Dkt. Jafo Aahidi Zahanati Kila Kijiji Kisarawe

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Seleman Jafo, ameahidi kuhakikisha kila kijiji katika wilaya hiyo kinakuwa na zahanati ili wananchi wapate huduma za afya karibu na makazi yao.

Akizungumza leo Septemba 09, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Kihale, Kata ya Marui, Wilaya ya Kisarawe, Dkt. Jafo alisema Kisarawe imekuwa wilaya ya kwanza katika Mkoa wa Pwani yenye idadi kubwa ya vituo vya upasuaji, na sasa anataka kupeleka mapinduzi ya huduma za afya kwa kuhakikisha kila kijiji kinajengewa zahanati yake.

Alisisitiza kuwa miradi hiyo itaambatana na ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya ili huduma zitolewe kwa ufanisi na kwa muda mrefu, na kuongeza kuwa lengo lake ni kuboresha maisha ya wananchi wa Kisarawe kupitia upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu na maendeleo ya kijamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!