Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera amewasili Nchini Geneva, Uswisi kuhudhuria Mkutano wa Ngazi ya Juu katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa linaloanza leo tarehe 23 Februari, 2026.
Katika kikao hicho, Mhe. Waziri anatarajia kuwasilisha taarifa ya Nchi juu ya hali ya Haki za Binadamu nchini.
Awali Mhe. Homera ametembelea Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania nchini Geneva ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na
Balozi na Dkt. Abdallah Possi ambaye ni Mwakilishi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Hoyce Temu.












