Home Biashara CBE YAKAMILISHA TAFITI 129, YAANZA NYINGINE

CBE YAKAMILISHA TAFITI 129, YAANZA NYINGINE

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kinaendelea kufanya tafiti zinazolenga kubaini na kutoa suluhisho kwa changamoto za biashara, uchumi na maendeleo nchini, huku tafiti 129 zikikamilishwa mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 14, 2026 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti, Machapisho na Ushauri wa Kitaalamu wa Chuo hicho, Prof. Nasibu Mramba, amesema tafiti mbili zinatarajiwa kuanza siku za karibuni, ikiwemo utafiti kuhusu biashara zisizo rasmi, hususan wamachinga.

Amesema utafiti mwingine utahusu mahitaji ya ujuzi katika viwanda, kwa lengo la kubaini aina ya wataalamu wanaohitajika na namna ya kuwaandaa, kutokana na baadhi ya viwanda kuajiri wataalamu kutoka nje ya nchi.

Prof. Mramba amesema tafiti saba zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika Januari, zikiwemo zinazohusu biashara katika mpaka wa Tunduma, soko la kokoa, uvuvi wa kibiashara katika Ziwa Victoria, wanawake wajasiriamali katika machimbo ya madini na kilimo cha zabibu katika Kanda ya Kati.

Amesema CBE pia inatarajia kuanza tafiti Dar es Salaam na Pwani zinazolenga changamoto za mikopo na masuala yanayowakabili wananchi, akisisitiza kuwa tafiti hizo zinalenga kupata suluhisho la changamoto za kibiashara na kiuchumi nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!