Home Biashara CBE YAPANUA FURSA ZA ELIMU YA JUU

CBE YAPANUA FURSA ZA ELIMU YA JUU

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kimepanua fursa za elimu ya juu kwa kutoa programu zinazolenga kuwaandaa wataalamu wenye ujuzi katika biashara, teknolojia na uongozi. Hatua hiyo inalenga kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Edda Tandi Lwoga, Septemba 14, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu programu zinazotolewa na chuo hicho.

Amesema miongoni mwa programu hizo ni Bachelor of Business Administration Double Degree, inayotolewa kwa ushirikiano na Southwestern University of Finance and Economics (SWUFE) ya China. Mwanafunzi husoma miaka miwili CBE na miaka miwili China na kupata vyeti kutoka vyuo hivyo viwili.

Amesema programu hiyo inawawezesha wanafunzi kupata ujuzi wa kusimamia biashara za ndani na kimataifa. CBE pia imeanza mwaka huu Bachelor Degree in Digital Technology Solution Management with Apprenticeship, kwa ushirikiano na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).

Katika programu hiyo ya miaka mitatu, mwanafunzi husoma muhula mmoja CBE na mwingine katika taasisi mshirika. Hii humwezesha kupata uzoefu wa kazi na kujifunza kutengeneza suluhisho za kidigitali.

Kwa elimu ya uzamili, CBE inatoa programu za Master of Information Technology Management, Master of International Business Management na Master of Supply Chain Management. Pia kuna MBA katika Human Resources Management, Banking and Finance na Marketing.

CBE pia inatoa Project Management na Master’s Degree in Leadership and Governance. Programu hizo zinalenga kuandaa wataalamu katika usimamizi, uongozi na utawala.

Prof. Lwoga amewataka wazazi, vijana na Watanzania kutumia fursa hizo. Amesema udahili wa Bachelor unaendelea hadi Septemba 21, 2026, huku Certificate na Diploma ukiendelea hadi Septemba 18, 2026.

Amesema CBE itaendelea kutoa elimu bora, kukuza tafiti zenye tija na kuimarisha mchango wake katika maendeleo ya uchumi na biashara nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!