Home Kitaifa BARRICK GOLD MINE YAPONGEZWA KWA ULIPAJI WA KODI MZURI

BARRICK GOLD MINE YAPONGEZWA KWA ULIPAJI WA KODI MZURI

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda ameupongeza uongozi wa mgodi wa kuchimba madini ya dhahabu wa Barrick kwa kuwa walipaji kodi wazuri wanaofuata sheria za nchi.

Ametoa pongezi hizo leo tarehe 09.10.2025 alipofanya ziara katika mgodi wa Bulyanhulu uliopo wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kuwapongeza, kuwashukuru na kusikiliza changamoto zao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Bw. Mwenda amesema mgodi wa Bulyanhulu licha ya kuwa walipakodi wazuri pia wameajiri idadi kubwa ya wafanyakazi ambao wanalipa kodi sambamba na wakandarasi pamoja na wazabuni wanaofanya nao kazi na kuchangia katika ulipaji wa kodi.

Ninyi ni walipakodi wazuri hivyo tunawapongeza na kuwashukuru pia tunawaomba muendelee kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya Taifa letu, na sisi tutaendelea kuwezesha biashara zenu ” amesema Bw. Mwenda.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bw. Leon Ebondo ameishukuru TRA kwa kufanya ziara mgodini hapo, kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.

Bw. Ebondo amesema mgodi wa Bulyanhulu umeajiri watumishi wa kudumu 1,510 huku ikifanya kazi na wakandarasi zaidi ya 2,000 ambapo pia wapo wananchi wanaotoka katika vijiji vinavyozunguka mgodi wamekuwa wakipata ajira za muda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!