Home Kitaifa AZAM MEDIA WAUNGANA NA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KUHAKIKISHA WANAPATA...

AZAM MEDIA WAUNGANA NA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KUHAKIKISHA WANAPATA CHUPA 5000 ZA DAMU

Na Magreth Mbinga

Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kushirikiana na Azam media kupitia redio ya U FM watahamasisha wananchi kuchangia damu kupitia sherehe zote za Kitaifa zitakazo kuwa zinafanyika kwa lengo la kuunga mkono Serikali kusaidia upati kanaji wa Damu ya kutosha ili kuokoa vifo vya mama wajawazito na watoto.

Hayo yamezungumzwa na Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Adbi Juma na kusema kuwa Azam media kwa kuona umuhimu wa Damu Salama wanaungana na Wizara ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa Damu Salama kuhamasisha wananchi .

Kama tunavyojua hatuna kiwanda cha kutengeneza Damu tunategemea kujitoa kwa watu hivyo Azam media watahamasisha kupitia vipindi vyao mbalimbali kwa kuanza na sikukuu ya Uhuru ambayo itafanyika Disemba 9,2022″ amesema Dkt. Abdi.

Pia Dkt. Adbi amesema Disemba 9 itafanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya Karume,Kigamboni karibu na Chuo Cha Mwalimu Nyerere,Kituo Cha Damu Salama Kanda ya Mashariki,Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Hospitali zote za Mikoa na katika Timu zote za Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam.

Januari 12,2023 katika sherehe ya Mapinduzi itafanyika katika Mkoa wa Mbeya,Sherehe ya Muungano ambayo itafanyika Aprili 24,2023 itafanyika katika Mkoa wa Kigoma,Agosti 8,2023 katika sherehe za nanenane uhamasishaji utafanyika Mkoa wa Morogoro, Oktoba 14,2023 katika kumbukizi ya kifo Cha Mwalimu Nyerere itafanyika Mkoa wa Mwanza na Kampeni itahitimishwa Disemba 9,2023 katika sherehe za Uhuru”amesema Dkt. Adbi

Aidha Mhariri U FM Ramadhani Tuwa amesema wao Azam media wameamua kubeba dhamana kuelimisha jamii kuhusu uchangiaji Damu Salama kuhakikisha watu wanakuwa Salama.

Tumekuwa tukiripoti matukio ya ajali,vifo vya akina mama wakati wa kujifungua Tanzania nzima vyombo vyetu vimesambaa huko kama wananchi hatufurahii kutangaza matukio ya vifo tu na watu wanahitaji kufanyiwa upasuaji Damu hakuna,tunahaja ya kutoa elimu kwa jamii” amesema Tuwa

Sanjari na hayo Afisa Mawasiliano Wizara ya Afya Catherine Sungura amesema kwa niaba ya Wizara na Serikali wanashukuru Azam media kupitia redio yao ya U FM kwa kujitolea kuweza kusaidia Serikali katika kuhamasisha uchangiaji wa Damu Salama.

Damu ni muhimu na kama Wizara ya Afya tuna hitaji Damu kuweza kusaidia watu wanaopata changamoto mbalimbali ikiwemo ajali kwahiyo Damu nyingi inahitajika katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya “amesema Sungura.

Vilevile Meneja Damu Salama Kanda ya Mashariki Dkt. Pendaeli ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuweza kuwapelekea wadau na wahamasishaji mbalimbali wa kuchangia damu pia amemshukuru Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa jinsi anavyowapigania kuweza kupata Damu ya kutosha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!