Na, Mwandishi wetu Tanga.
Wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama ambao pia ni wakuu wa wilaya ndani mkoa wa Tanga wametakiwa kuendelea kuratibu mpango wa uhamasishaji wananchi kuhusu urasimishaji wa silaha kwa hiari zoezi ambalo linaendelea nchi nzima huku pia wakitakiwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari katika kampeni hiyo.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Sulumbu wakati akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba katika warsha ya uzinduzi wa semina elekezi kwa maafisa wa jeshi la Polisi ,watendaji na Wenyeviti wa mitaa kuhusu kampeni ya usalimishaji wa silaha kwa hiari ambapo serikali inaendeshwa zoezi Hilo kwa kushirikiana na umoja wa nchi huru za Afrika (AU) kwa kushirikiana na umoja wa mataifa (UNODA).



“Suala la ulinzi na usalama ni muhimu katika maendeleo ya mtu moja mmoja na taifa kwa ujumla ,silaha haramu zikibaki mikonono mwa halifu zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuvuruga umoja amani na hivyo kuhatatisha kukua kwa uchumi wa taifa silaha haramu pamoja na Mambo mengine husababisha migogoro , mauaji na Makosa makubwa ” alisema
“Mkoa wa Tanga utahakikisha unasimamia Hali ya Usalama wa watu wake kwa kuzingatia kuwa utawala Bora ni njia ya kuchangia kukua kwa uchumi Wenyeviti wote wa Kamati za ulinzi na usalama kuratibu mpango wa uhamasishaji wa wananchi kuanzia ngazi ya wilaya Hadi vitongoji, uhamasishaji pia ufanyike kwa kuwashirikisha viongozi wa dini lakini pia kupitia mikusanyiko vya kijamii na kubadika matangqzo sehemu za mikusanyiko” alisema Kanali Sulumbu.
Awali akizungumza kamishina msaidizi wa Polis na mkuu wa wa kitengo Cha usimamiizi na udhibidi wa silaha na leseni kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi Renarda Milanzi amesema kuwa katika kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama hapa nchini hatua za maksudi zimechukuliwa kwa kushirikiana makundi mbalimbali katika kutekeleza kampeni hiyo baada ya serikali kutoa tangqzo la msamaha kwa yeyote atakayesalimisha silaha kwa hairi hatoshitakiwa.

“Jukumu la usalama ni la kila mwananchi hivyo Basi Polisi kwa kushirikiana na wadua wa ndani na nje kimeona umuhimu wa kuwashirikisha makundi mbalimbali katika jamii ili kutekeleza kampeni ya mwezi wa msamaha wa kurasimisha silaha kwa hairi ili kuimarisha usalama wa Taifa letu kampeni hii inaendelea nchi nzima na atakayesalimisha hatoshitakiwa ” alisema Milanzi.
“Kampeni ya urasimishaji wa silaha inaendelea nchi nzima mkoa wa Tanga Morogoro na Tabora ilichaguliwa Kama mikoa darasa ya Kama mfano ili kuiwezesha mikoa mingine kujifunza kutokana na matokeo chanya yanayotarajiwa kupatikana hivyo ni wajibu wetu sote kuhakikisha kampeni hii inafanyika kikamilifu” aliongeza
“Hapa nchini hii ni mara ya pili kufanyika kwa mwezi wa Afrika ambapo November 2021 ndio ilikuwa mara ya kwanza nchi yetu kutangazwa msamaha wa kusalimisha silaha haramu na mwaka huu msamaha umetolewa kwa kipindi cha miezi miwili ili kutoa fursa kwa wananchi wanaomiliki silaha na hivyo kujitokeza kwa wingi kushiriki ili tuondoe uzagaaji wa silaha katika jamii zetu baada ya kipindi cha usalimishaji kuisha silaha hizo zitakusanywa ifikapo November 22.” aliongeza
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga ACP Safia Jongo alibainisha kuwa kumekuwa na matukio mbalimbali yanayohusishwa na matumizi ya silaha kinyume cha sheria ikiwemo mauaji ya wanyama na mengine ya kiuhalifu ambapo katika jitihada walizoendelea kuzichukuwa walifanikiwa kukamata silaha 62 na na watuhumiwa 63 wakikamatwa kwa kipindi cha kuanzia January Hadi june 2022.

Jongo alisema kufwatilia uzagaaji wa silaha Tanga ni miongoni mwa mikoa mabayo unaweza kuathirika moja kwa moja katika mauaji na uwindaji haramu wa wanyama mbalimbali .
“Tanga itakuwa ni moja wapo ya mikoa ambayo itaathirika endapo kutakuwa na uzagaaji wa silaha kwani kutakuwa na vitendo vya uhalifu Kama mauaji na uwindaji haramu, mapori yetu mengi Yana wanyama silaha hizo zimekuwa zikitengenezwa kienyeji , kwahiyo urasimishaji wa silaha utatusaidia na utajisaidia mwenyewe na kjisaidia jamii kwa sababu kumiliki silaha visivyo halali utafanya matendo ambayo yatatuletea shida Kama uhalifu wa wanyama na matukio mengi ambayo yanatumia silaha” alisema Jongo.
Zoezi hilo ambalo ni kwa mara ya pili kufanyika hapa nchini kuanzia mwaka huu lilizinduliwa na Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Jumaanne Abdallah jijini Dodoma September 1 ambapo litendelea hadi October 31 , 2022.
MWISHO.








