Home Kitaifa AFISA MIPANGO MIJI MBARONI KWA KUDAIWA KUMBAKA MTOTO

AFISA MIPANGO MIJI MBARONI KWA KUDAIWA KUMBAKA MTOTO

Na Neema Hussein, KATAVI

Jeshi la Polisi mkoani Katavi linamshikilia Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Mpimbwe Dickson Mwenda (37) kwa tuhuma za kudaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkazi wa Kibaoni.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Ali Makame amesema mtuhumiwa anadaiwa kumbaka mtoto huyo ndani ya gari yake yenye namba za usajili T 927 DMC.

Kamanda Makame alieleza kuwa tukio hilo la unyanyasaji wa kingono lilifanyika tarehe 13 mwezi huu majira ya saa moja na nusu jioni huko katika Kijiji cha Kibaoni, kata ya Kibaoni.

Aliongeza kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa baa akipata vinywaji na mtuhumiwa ambapo baada ya muda alimuomba awapeleke watoto wake nyumbani ambao walikuwa wawili yaani mtoto aliyebakwa na mdogo wake.

Alieleza kuwa mtuhumiwa alipofika njiani alisimamisha gari na kumnajisi mtoto huyo.

Alisema kuwa baada ya tukio hilo taarifa zilipelekwa kituo cha Polisi na baadae mtuhumiwa alikamatwa.

Kamanda Makame alisema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na polisi na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakama kujibu tuhuma zinazomkabili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!