Home Kitaifa CPC WAWEZESHA VIJANA 50 KUTAPATA MAFUNZO SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU NYERERE...

CPC WAWEZESHA VIJANA 50 KUTAPATA MAFUNZO SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU NYERERE KIBAHA PWANI

Na Scolastica Msewa, Kibaha.
CHAMA Cha Kikomunisti cha nchini China CPC kimetoa ufadhili wa mafunzo mafupi ya siku kumi kwa wanachama 50 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Umoja wa Vijana na UWT ambao wamechaguliwa kote nchini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo masuala ya Siasa, uchumi na mkakati wa kuendeleza mahusiano kati ya nchi ya China na Tanzania.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu CCM bara comredi Anamringi Macha katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani amesema kuwa mafunzo haya ni mahsusi kwa ajili ya kuwajengea uwezo Viongozi ili na wao waweze kwenda kutoa elimu ya mafunzo watakayo yapata baada ya kuhitimu.

Macha amesema kuwa viongozi hao watapata fursa ya kupewa mafunzo hayo kupitia wawezeshaji Viongozi Wasomi wabobezi na wanazuoni ambao ni viongozi wakongwe katika historia ya nchi kwa kufanya kazi kwa miaka mingi serikalini ili wawafundishe viongozi hao uvumilivu katika kulitumikia taifa.

Amewataja Wawezeshaji hao kuwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na Katibu Mkuu kwa kipindi cha miaka kumi,pia alikua Mkuu wa Chuo Cha CCM Kivukoni Kivukoni Mzee Philip Makula, Komredi Stephen Wassira, alikuwa Naibu Katibu Mkuu Visiwani CDE Abdallah Mabodi, Prof. Samuel Wangwe , Prof. Paramagamba Kabudi, Kanali Mstaafu Simbakalia,

Aidha katika mafunzo haya wakufunzi kutoka CPC watatoa mada ya mahusiano ya nchi mbili hizi katika sekta ya uongozi, kibiashara, mahusiano na ushirikiano wa China kiuchumi, na siasa ili waweze kuiva na kuwa mabalozi katika kizazi hiki na kijacho.

“Tutawafundisha mbinu kwa nini CPC wameweza kudumu na kuwa chama kikongwe kilichodumu madarakani kwa miaka 100 tangu kilipoanzishwa” alisema.

Aidha alisema Viongozi hao watafundishwa masuala ya maendeleo, mafanikio ya nchi ya China kwa sasa na mikakati iliyopo kuelekea miaka ijayo.

Ameongeza kuwa CCM kimewakusanya viongozi hao wa UVCCM na UWT ili kuendelea kuwafunda vijana wake ili watambue nini cha kufanya kwa Taifa badala ya kuendelea kutegemea taifa liwafanyie kitu.

“Moja ya matatizo makubwa kwa vijana wetu sasa hivi wanakukosa uvumilivu wanaingia katika maeneo wakitaka mambo yabadilike kwa haraka yakiwahusu wao kwahiyo tunapowaweka hapa ni kama kuwafunda na kuwaeleza umuhimu wa uongozi” alisema

Alisisitiza kwamba viongozi wataendelea kuwaweka vijana kwenye nafasi za uongozi na kwamba mabadiliko ya nafasi yanapotokea ni kutaka kuona nani anafaa kwenye hiyo nafasi katika utendaji na kuleta maendeleo.

Hatahivyo Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM bara ameonya tabia ya baadhi ya viongozi vijana kulewa kuacha madaraka na badala yake wametakiwa kufanyakazi Kwa weledi.

Alisema baadhi ya viongozi vijana wa sasa wengi wamekuwa sio wavumilivu na kwamba baadhi ya nafasi za uongozi walizonazo wamekuwa wakizitunia vibaya na kwamba CCM haita sita kuwaondoa na kuwachukulia hatua.

“Lazima tuwe wakweli tatizo tulilonalo Sasa hivi vijana wanakosa uvumilivu wanaingia kwenye uongozi na kutaka mambo kubalika Kwa haraka..wengine wanalewa madaraka Kwa badala ya kutumia nafasi Kwa kazi iliyokusudiwa akaanza kufanya vitu sivyo, mtu huyo hatuwezi kumuacha tutamuondoa” alisema

Aidha alisema lengo la Chama Cha Mapinduzi ni kuwalea vijana na kuwa viongozi Bora na kwamba mafunzo hayo yanalengo la kuwafunda kiungozi na wanawajibu wa kulifanyia taifa mambo makubwa.

Aidha Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Baraza la Umoja wa Wanawake Taifa (UWT), Mariamu Ulega amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha hayo mafunzo hii ni fursa kubwa kwa wanawake kwa sababu ukimuelimisha mwanamke umeielimisha jamii nzima hivyo elimu hiyo watakayoipata watakwenda kuipeleka kwa jamii hususan katika ziara mbalimbali ambazo zinafanywa UWT.

Kama sasa hivi kumekua na ziara zinazoendelea kupitia Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda ambapo wanapita kufanya mikutano mbalimbali katika ngazi za Kata, Vijiji na Mkoa.

Akizungumzia kuhusu chaguzi za serikali za mitaa mwakani amesema kuwa wanawake wajitokeze kuchukua fomu za kugombea na wanawake wengine wawasapoti kuwasaidia ili waweze kushinda” amesema Mariam.

Mariam aliwakumbusha wananchi kujitokeza kwenye mikutano mbalimbali ya chaguzi zijazo na kusikiliza sera za chama na kukipa nafasi zaidi CCM.

Naye mshiriki wa mafunzo hayo Mhandisi Fatma Rembo amesema kuwa anategemeakuwa baada ya kupata mafunzo haya wanatarajia kuja kuwa viongozi bora zaidi kwa kuliongoza taifa.

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa SUKI Rabia Abdallah Hamid alishukuru Chama Cha CPC kwa uwezeshaji wa Mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na uwekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

++++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!