Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, Mkaguzi wa Jeshi la Polisi (Insp) Hosiana Mushi, Octoba 6, 2023 akitoa elimu na kumpongeza dereva bodaboda kwa kuwa mfano bora wa kufuata sheria za usalama barabarani.
Insp Hosiana amempongeza pia dereva huyo kwa kujali maisha ya abiria wake kwa kumvisha kofia ngumu. Aidha, bodaboda huyo amekuwa mfano bora kwa kutii amri ya askari ya kusimama baada ya kusimamishwa ili akaguliwa.
“Tanzania bila ajali inawezekana, Timiza wajibu wako”








