Home Afya MADAKTARI BINGWA KUTOKA UJERUMANI KUWASILI TANGA JULAI 13, KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA

MADAKTARI BINGWA KUTOKA UJERUMANI KUWASILI TANGA JULAI 13, KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA

Na Boniface Gideon- TANGA

MADAKTARI Bingwa kutoka Nchini Ujerumani wanatarajiwa kuwasili Mkoani Tanga Julai 13 mwaka huu ambao wanakuja kwa ajili ya kutoa huduma za Kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Tanga jana,Mratibu wa Kambi ya Upasuaji wa Kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery) kwenye Hospitali hiyo Dkt Wallace Karata alisema watakuwepo hadi Julai 28 mwaka huu na siku inayofuatia wataondoka nchini.

Dkt Karata alisema kwamba madaktari hao wanakuja kutoa huduma kwa watanzania ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu lakini pia kwa fani yao ya upasuaji na kurekebisha maumbile ambayo haipatikani vya kutosha nchini na hivyo wanakuja kutoa bure kama msaada kwa watanzania.

Alisema hadi sasa wagonjwa 200 wamekwisha kujiandikisha na wakiwa tayari kwa ajili ya kusubiri huduma na Julai 10 ilikuwa ni mwisho kujiandikisha na wageni hao watakapoingia Julai 14 watafanya uchunguzi wa awali na kuweza kupanga ratiba za upasuaji.

Dkt Karata alisema operesheni zitaanza Julai 17 hadi Julai 28 kabla ya wageni hawajaondoka nchini hivyo waliojiandikisha wasishaua tarehe waliozopewa ili kuepukana na usumbufu wa kupanga ratiba zao.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!