Home Kitaifa RC MTANDA ATAKA UKATILI DHIDI YA WAZEE UDHIBITIWE

RC MTANDA ATAKA UKATILI DHIDI YA WAZEE UDHIBITIWE

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara,Said Muhamed Mtanda, amesema wazee wanapaswa kupewa huduma stahiki na kudhibiti masuala ya ukatili dhidi yao.

Kauli hiyo ameitoa wakati alipokutana na wazee wa mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa uwekezaji katika kujitambulisha kwao.

Amesema kabla ya kuendelea na majukumu yake kama mkuu wa mkoa ameamua kukutana na wazee ili apate baraka zao na kuwasikiliza.

Mtanda amesema wazee wanastahili kuhudumiwa zikiwemo huduma za afya na kuto hudumiwa kwa ufanisi ni moja ya ukatili wanaofanyiwa wazee.

Amesema kwenye zahanati,vituo vya afya na hospital kunapaswa kuwa na madilisha maalumu ya kuwahudumia wazee wanapofika maeneo hayo.

Kabla ya kuendelea na majukumu yangu nimeona nikutane na wazee wangu ili nipate baraka zenu na kuwasikiliza namna gani tutafanya kazi hapa mkoani Mara.

Wazee wanapaswa kuhudumiwa kuanzia ngazi ya familia na kwenye ofisi za umma na taasisi binafsi na wasipohudumiwa huo ni ukatili na lazima udhibitiwe”,amesema Mtanda.

Katibu wa baraza la wazee mkoa wa Mara,Amina Magoti,amemshukuru mkuu wa mkoa wa Mara kwa kuamua kukutana na wazee na kuwasikiliza

Amesema juni 15 itakuwa siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee na kuomba wazee wawezeshwe kufika wilayani Bunda ili kushiriki maadhimisho hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!