Home Kitaifa  Ewura Yaimarisha Uelewa Wa Watendaji Wa Mkalama Kuhusu Udhibiti Wa Nishati Na...

 Ewura Yaimarisha Uelewa Wa Watendaji Wa Mkalama Kuhusu Udhibiti Wa Nishati Na Maji

Celebrating 25 Years of NHIF

Na.Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kupitia EWURA Kanda ya Kati, imetoa elimu kwa viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa na Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, kuhusu majukumu ya Mamlaka na taratibu za udhibiti wa huduma za nishati na maji.

FAHARI AFYA

Elimu hiyo imetolewa leo, Novemba 27, 2026, kupitia semina iliyoongozwa na Meneja wa EWURA Kanda ya Kati, Bi. Hawa Shani Lweno, ikiwa na lengo la kuongeza uelewa wa washiriki kuhusu huduma zinazodhibitiwa na kuwawezesha kutoa elimu sahihi kwa wananchi katika maeneo yao.

Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ni majukumu ya EWURA na udhibiti wa sekta zinazodhibitiwa, utaratibu wa kupata leseni za biashara ya mafuta kwa rejareja katika maeneo ya mijini na vijijini, umuhimu wa uvunaji na matumizi ya maji ya mvua, pamoja na utaratibu wa kupata leseni za ufungaji wa mifumo ya umeme.

Aidha, washiriki walipata elimu kuhusu namna EWURA inavyopokea na kushughulikia malalamiko na migogoro inayohusu huduma zinazodhibitiwa, ikiwemo taratibu za kuwasilisha malalamiko hayo.

Semina hiyo imewashirikisha watendaji kutoka ngazi za vijiji, kata, wilaya na mitaa pamoja na wawakilishi wa wananchi, ambao ni wadau muhimu katika kufikisha elimu ya udhibiti kwa jamii, kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao na kuhakikisha wanapata huduma bora za nishati na maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!