Home Kitaifa RAIS DKT. MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA KOREA KUSINI KUWEKEZA ZANZIBAR

RAIS DKT. MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA KOREA KUSINI KUWEKEZA ZANZIBAR

Celebrating 25 Years of NHIF

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewakaribisha wawekezaji wa Korea Kusini kuwekeza Zanzibar katika sekta mbalimbali za kiuchumi, huku akiwahimiza kuanzisha ubia na wafanyabiashara wa ndani kwa lengo la kuongeza mitaji, kuleta teknolojia mpya na kukuza biashara.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 30 Oktoba 2026, katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, iliyofanyika katika Hoteli ya Grand Hyatt, jijini Seoul, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Korea Kusini.

FAHARI AFYA

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema Zanzibar ina fursa kubwa za uwekezaji katika sekta za Uchumi wa Buluu, utalii, bandari, usafirishaji na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, huku Serikali ikiendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kupitia sheria, kanuni na huduma za Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

Amewahimiza wawekezaji wa Korea Kusini kushirikiana na kampuni za Zanzibar ili kuunganisha mitaji, teknolojia na uzoefu kwa manufaa ya pande zote mbili.

Rais Dkt. Mwinyi amekamilisha ziara yake nchini Korea Kusini, iliyohusisha mikutano ya uwekezaji na biashara jijini Seoul, ziara za viwanda na miradi jijini Yeosu, ushiriki katika Mkutano wa ITOP visiwani Jeju, pamoja na mazungumzo na makampuni ya Korea kuhusu fursa za miradi ya kimkakati Zanzibar.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wawakilishi wa Serikali ya Korea Kusini, wanadiplomasia, viongozi wa taasisi za fedha, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka sekta mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!