

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço, leo Oktoba 30, 2026, wamezindua barabara za lami zenye urefu wa kilomita 59.1 zilizojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Barabara hizo zilizojengwa na TARURA, kilomita 11.2 ni za njia nne zenye upana wa mita 7 kila upande (Dual Carriageway), na kilomita 36.7 ni za njia mbili zenye upana wa mita 7.
Barabara hizo pia zina mabega yenye upana wa mita 0.9 kila upande, njia za waenda kwa miguu zenye upana wa mita 1.5 kila upande na njia za baiskeli zenye upana wa mita 2.7 kila upande.
Pia, limetengwa eneo lenye upana wa mita 4 kila upande kwa ajili ya kuweka huduma za maji safi na taka, umeme, gesi na TEHAMA.









