Home Kitaifa TCDC YASHIRIKI MASHINDANO YA RIADHA

TCDC YASHIRIKI MASHINDANO YA RIADHA

Wanamichezo wa TCDC Sports Club wameshiriki mashindano ya riadha (mbio) katika Michezo ya kitaifa Meimosi inayoendelea mkoani Njombe.

Wachezaji walioshiririki mbio hizo ni Mbaso John aliyekimbia Mita 100 na kuibuka mshindi wa tatu (3) katika round ya kwanza, na baadae kupoteza nafasi ya ushindi katika hatua ya nusu fainali.

Mchezaji mwingine ni William Valentine aliyeshiriki riadha mbio za Mita 800 na kutofaninikiwa kupata ushindi baada ya kuzidiwa na wanariadha kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Wizara ya Mambo ya ndani.

Kwa upande wake Noel Steven ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCDC Sports Club ameshiriki mchezo wa Draft ambapo kwa mzunguko wa kwanza TCDC Sports Club ilishinda mechi mbili na mzunguko wa pili kupata draw na hivyo kutofanikiwa kuvuka hatua za makundi baada ya kuzidiwa kete na TRA na Wizara ya Kilimo.

Michezo hiyo yote imechezwa Aprili 21, 2026 katika viwanja vya Njombe Sekondari na Viwanja vya sabasaba (77) mkoani humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!