Home Kitaifa PROF. CHANDE AKAGUA JENGO LA VIWANGO HOUSE DODOMA

PROF. CHANDE AKAGUA JENGO LA VIWANGO HOUSE DODOMA

Na Mwandishi Wetu – Dodoma 

Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la viwango Tanzania  (TBS), Prof. Othman Chande Othman leo Aprili 15,2026 amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi  wa Viwango House  Dodoma linalojengwa katika eneo la  Njedengwa Jijini Dodoma ambapo kwasasa umefikia  asilimia 97% kukamilika.

Prof. Chande amesema kupitia ukaguzi walioufanya wamejilidhisha na kazi iliyofanywa na mkandarasi.

“Jengo hili likikamilika litasaidia sana watu wa kanda ya kati pamoja na kanda ya magharibi, kwasababu itakuwa sasa sample zao zote ambazo sisi kwa kawaida tunapima Dar es Salaam tutaweza kuzipimia Dodoma,”amesema. 

Amesema kupimiwa kwa sampuli hizo Dodoma kutapunguza wakati wa kupata majibu kutoka TBS, hatua itakayofanya wafanyabiashara kufanya kazi kwa weledi zaidi.

Katika hatua nyingine Prof. Chande amesema TBS inawawezesha wafanyabiashara kuuza bidhaa zao sehemu mbalimbali ili viweze kuuzika kwa usalama zaidi. 

Kwa upande wa wasimamizi wa mradi huo kupitia kwa Mhandisi Johnson Malisa amesema mradi huo utarajiwa kukabidhiwa hivi punde  ambapo kazi zote zilizosalia zitakuwa zimekamilika.

“Mradi huu una malengo ya kuhudumia kanda ya kati kwa Mikoa ya Singida na Dodoma ambapo linajumuisha ofisi na maabara mbalimbali kwaajili ya vipimo vya vifaa mbalimbali vinavyozalishwa nchini, “amesema. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!