Home Kitaifa REA YATOA ELIMU YA UMEME MKOANI TANGA

REA YATOA ELIMU YA UMEME MKOANI TANGA

Wakala wa nishati vijijini (REA) umeendelea na zoezi la uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya umeme.

Uhamasihaji umefanyika wilayani Pangani ambapo maafisa wa REA na TANESCO wametembelea nyumba ambazo zimenufaika na miradi ya umeme pamoja na kufanya mikutano ya hadhara yenye lengo kuu la kuwapa uelewa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na huduma ya umeme.

Akizungumza wakati wa uhamasishaji Afisa maendeleo ya jamii kutoka REA , ndugu Abdulrazack Mkomi amesema,

Kwa sasa taratibu za uombaji huduma ya umeme zimeboreshwa zaidi na hakuna tena mambo ya kutumia fomu kufanya maombi ambapo kwa kutumia tu namba ya Nida mwananchi anaweza kufanya ombi la umeme moja kwa moja TANESCO kupitia huduma ya NIKONEKT.

Kwa kutumia simu janja, mwananchi atapakua huduma ya Nikonekt na kufanya maombi au kama ni simu ya kawaida atabonyeza 15200# na kisha kufuata maelekezo ya kufanya ombi, hakuna mawakala wanaosajili maombi mtaani tafadhali tuepuke vishoka” mkomi alisisitiza.

Aidha mkomi ameongezea kuwa, pamoja na umeme kufika majumbani ni vyema wananchi walio eneo la mradi wakachangamka na kutumia fursa hiyo kujiunga mapema na huduma ya umeme.

Aidha, wananchi wameombwa kuendelea kutunza miundombinu ya umeme kwani mpaka umeme unafikishwa katika kijiji na au kitongoji umesafiri kutoka mbali sana na umepita katika njia salama ndio maana unawaka, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kulinda na kutunza miundombinu ya umeme ili kuhakikisha usalama muda wote.

Halikadhalika, uelimishaji huu utaendelea wilaya kwa wilaya, Kata kwa kata kijiji kwa kijiji na kitongoji kwa kitongoji mkoani Tanga.

Vilevile, REA itaendelea kutekeleza na kusimamia miradi tofauti tofauti ya umeme ikiwemo miradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji na na miradi ya ujazili ili kuhakikisha kila mwananchi wa mkoa wa Tanga hususani mwananchi aishie kijijini na pembezoni mwa jiji anafikiwa na huduma ya umeme.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!