Home Kitaifa RAIS DKT SAMIA KUZINDUA SOKO LA KARIAKOO FEBRUARI 08, 2026

RAIS DKT SAMIA KUZINDUA SOKO LA KARIAKOO FEBRUARI 08, 2026

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua soko la Kariakoo Februari 8, 2026 ambalo lilikuwa kwenye ukarabati baada ya kuungua na moto na Soko jipya ambalo limejengwa

Akizungumzia ujio wa Rais Dkt Samia RC Chalamila amesema soko hilo kwa sasa limekamilika kwa asilimia 100 ambapo zaidi ya shilingi bilioni 28 zimetumika kukarabati na kujenga soko jipya likiwa na takribani vizimba zaidi ya 1500 kwa ajili ya wafanyabiashara

RC Chalamila amewataka wananchi wakazi wa Mkoa huo, wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa kujitokeza kwenye uzinduzi huo wa Soko la kariakoo ili kumuunga mkono Rais Dokta Samia lakini pia kuweka historia ya tukio hilo kubwa linalotarajiwa kuwa ni kiungo muhimu katika kujenga uchumi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla

Aidha Chalamila ameagiza wafanyabiashara wadogo ambao wamefunga barabara za kuingia soko la kariakoo waondoke na waache barabara hizo wazi kabla ya februari 8 ili kuruhusu wafanyabiashara kuingia kwenye Soko hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!