Home Kitaifa PAPA AKEMEA MATUMIZI YA DINI

PAPA AKEMEA MATUMIZI YA DINI

Viongozi wa siasa pamoja na wa kidini wanaotumia imani kama chombo cha kuidhinisha migongano, mapambano au sera za utaifa wamekosolewa vikali na Kanisa Katoliki duniani kupitia kiongozi wake Papa Leo, Alhamisi Desemba 18, 2025, akieleza kuwa hatua hiyo ni kosa kubwa la kiimani linalokiuka heshima ya Mungu.

Ujumbe huo umetolewa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani yatakayofanyika Januari Mosi, 2026, ambapo hakumtaja mtu yeyote kwa jina, bali aliwahamasisha waumini kupinga matumizi yasiyo sahihi ya dini katika uwanja wa kisiasa.

Ameeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona misamiati ya kiimani ikivutwa kwenye mvutano wa kisiasa, kuhalalisha misimamo ya utaifa na kutoa uhalali wa machafuko pamoja na mapigano ya silaha kwa kisingizio cha imani.

Papa Leo ameonya kuwa baadhi ya viongozi wa kidini hutumia nafasi zao kuchochea chuki miongoni mwa waumini, huku wakijaribu kuhalalisha hali hiyo kama uzalendo, akisisitiza kuwa waamini wanapaswa kupambana na mwenendo huo kupitia vitendo na mwenendo wao wa kila siku.

Katika ujumbe huo wa kila mwaka, Papa Leo pia ameonesha hofu juu ya kuongezeka kwa matumizi ya silaha duniani, akirejea takwimu za Taasisi ya Stockholm ya Utafiti wa Amani (SIPRI) zinazoonesha kupanda kwa matumizi ya kijeshi mwaka 2024 na kufikia Dola za Marekani trilioni 2.7, sawa na asilimia 2.5 ya Pato la Taifa la Dunia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!