Home Kitaifa WATUHUMIWA 24 MBARONI TUHUMA ZA UHALIFU

WATUHUMIWA 24 MBARONI TUHUMA ZA UHALIFU

Na Magrethy Katengu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata Mohamed Amani (45) “kiziwi”, mkazi wa Dar es Salaam na Mwanza pia Salome Richard (32) mama “G” mkazi wa Mwanza na wengine wanane kwa tuhuma za wizi wa magari katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Jijini Dar es salaam Kamanda wa JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro amesema Katika Operation hiyo kali, iliyofanyika magari 23 aina mbalimbali, ambayo ni IST 5, fuso 1, Nissan Civilian 1, Coaster 1, Toyota Hilux pickup 1, Nissan patrol 1, Toyota Premio 2, Probox 1, Spacio 2, Harrier 2, Ravfour 3, Town Hiace 2 na Hiace 1, yalikamatwa katika Mikoa ya Mwanza, Iringa, Kilimanjaro, Kagera, na Dar es Salaam.

Pichani Kamanda wa Mkoa wa Dar es salaam Jumanne Muliro akionyesha Magari yalioibiwa na kubandikwa namba feki

Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi baada ya mahojiano na watuhumiwa hao ilibainika kabla ya kuiba huvizia magari hayo yakiwa yameegeshwa kwenye maegesho ya jumla, binafsi na majumbani baadae kuvunja vitasa vya milango ya upande wa dereva na kuwasha gari kwa kutumia fungo bandia Kisha ukondoka nayo kuyauza mikoani.

Hata hivyo Jeshi lilibaibi kuwa watuhumiwa hao baada ya kuiba magari hayo hubandika namba za usajili na chasses za magari yaliyopata ajali na kuuzwa kama vyuma chakavu na makampuni ya bima baadae kuyauza tena magari hayo ya wizi hivyo baadhi ya magari yameshatambuliwa na wamiliki na upelelezi unaendelea.

Huwezi kukimbia Jeshi la polisi ukiwa umefanya tukio kwani tunashirikiana vizuri tutakukamata popote ulipo tumejipanga kudhibiti uhalifu kama unafikiria wewe ni mjanja wa mbio unajidanganya tuko macho” amesema ACP Jumanne

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi linawashililia akam watuhumiwa sita(majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) kwa tuhuma za wizi wa vifaa mbalimbali vya miundombinu ya TANESCO vinavyotumika katika ujenzi umeme wa msongo wa kati (REA).

Watuhumiwa hao walikamatwa Octoba 6 mwaka huu majira ya saa nane mchana maeneo ya Mwenge, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa na vifaa mbalimbali vya miundombinu ya TANESCO kwenye gari aina ya Noah yenye namba za Usajili wa T 165 DPR.

Upelelezi wa Jeshi la Polisi umebaini kwamba vifaa hivyo ambavyo ni mali ya kampuni ya State Grid Electrical and Technical LTD na Tropical Industrial LTD viliibwa Mkoa wa Morogoro na Lindi, na watuhumiwa hao walikuja Dar es Salaam kwaajili ya kutafuta soko” Amesema Kamanda Muliro.

Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kuwa halitamvumia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kukwamisha maendeleo kwa miradi hiyo imejengwa kwa manufaa ya Umma. Ufuatiliaji na uchunguzi wa kina unaendelea.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia jumla ya Walimu 14 kwa tuhuma za kukiuka sheria, kanuni, na taratibu mbalimbali za mitihani ya darasa la saba iliyofanyika tarehe 5-6 mwezi wa 10, 2022. Uchunguzi wa suala hili unaendelea na taarifa zitatolewa na mamlaka zinazohusika na masuala ya elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!