Home Kitaifa WANANCHI IGUNGA WAAHIDI KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME NA KUTUMIA NISHATI SAFI...

WANANCHI IGUNGA WAAHIDI KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME NA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Celebrating 25 Years of NHIF
📌 Sasa Umeme ni Kitongoji kwa Kitongoji
📌 Nishati Safi ya Kupikia kwa Kila Mtanzania

Wananchi wa vijiji vya Maguguni, Lubeho na Mwama Bogo, Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora, wameahidi kujiunga na huduma ya umeme na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia baada ya kupatiwa elimu kuhusu umuhimu na manufaa ya matumizi ya nishati hizo na wataalamu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Ahadi hizo zimetolewa kufuatia ziara ya wataalamu wa REA waliotembelea vijiji hivyo na kufanya mikutano na wananchi kwa lengo la kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya umeme pamoja na nishati safi ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha upatikanaji na matumizi ya nishati bora kwa wananchi wanaoishi vijijini.

FAHARI AFYA

Kupitia mikutano hiyo, wananchi wamepata fursa ya kuelewa manufaa mbalimbali yatokanayo na upatikanaji na matumizi ya umeme, yakiwemo kukuza shughuli za kiuchumi, kuongeza fursa za uzalishaji mali, kuboresha huduma za kijamii na kuimarisha usalama katika maeneo wanayoishi.

Aidha, wananchi wameelimishwa kuhusu taratibu za kuomba kuunganishiwa huduma ya umeme, gharama za kuunganishiwa, umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme pamoja na kuzingatia tahadhari za kiusalama wakati wa matumizi ya nishati hiyo ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na matumizi yasiyo sahihi.

Katika hatua nyingine, wananchi hao wamepatiwa elimu kuhusu umuhimu na manufaa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa afya, mazingira na uchumi. Elimu hiyo imehusisha matumizi ya vifaa mbalimbali vya nishati safi ya kupikia, ikiwemo majiko ya umeme, kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuongeza matumizi ya nishati safi na kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi zinazoweza kuathiri afya ya binadamu na mazingira.

Vilevile, wananchi wamehimizwa kutumia fursa ya upatikanaji wa umeme vijijini kuanzisha na kuimarisha shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazotumia nishati hiyo, hatua inayotarajiwa kuongeza kipato cha kaya na kuchochea maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Utoaji wa elimu hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kupitia REA za kuendelea kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi wanaoishi vijijini kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati ya kisasa, salama na endelevu, kwa lengo la kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kunufaika na fursa zinazotokana na upatikanaji wa nishati.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!