Home Burudani WAKUMBUSHIA AHADI YAO KWA RAIS SAMIA

WAKUMBUSHIA AHADI YAO KWA RAIS SAMIA

Na Theophilida Felician Kagera.

Albert Christan Kahabuka ambaye ni mlevu wa viongo vya mwili ambayo ni miguu na Novati Joseph Mwijage mlevu wa kutokuona wakazi wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera pia wasanii wa mashairi na nyimbo kadha wa kadha wameomba na kukumbushia kutimiziwa ahadi waliyoahidiwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya kusaidiwa kuungwa mkono katika kurekodi na kutengeneza kazi zao kwenye studio za kisasa ili ziweze kuwa katika viwango vizuri na vyenye tija zaidi.

Wawili hao wakizungumza na Mzawa Blog maeneo ya kata ya Kagondo Manispaa ya Bukoba wamesema kuwa Rais Samia alitoa ahadi hiyo baada ya wao kushiriki nakuimba kwenye sherehe za kuhitimisha kilele cha mbiyo za Mwenge wa Uhuru Mnamo Tarehe 14 October/ 2022 katika viwanja vya Kaitaba Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Wamefafanua kuwa baada ya Rais Samia kushuhudia ukali wa kazi zao aliwiwa nakutoa ahadi hiyo ambayo haijatekelezeka tangu kipindi hicho mpaka sasa.

Wameeleza kuwa wamekuwa wakifuatiria suala hilo maeneo mbalimbali bila ya mafanikio ambapo wamewahi kuwasiliana na naibu waziri wa ofisi ya waziri, Mkuu kazi,vijana, ajira, na watu wenye ulemavu Patrobas Paschal Katambi ambaye aliwajibu kuwa tayari jambo hilo alikwishalielekeza wizarani kwa mtu mmoja wa wizara hiyo ambaye ni Eliakimu Mtawa aliyepokea barua yao ya ukumbusho wa ahadi hiyo kwanjia ya Email.

Wamesema kuwa licha ya jitihada hizo hadi sasa hawajawahi kupata majibu sahihi ya kutimiziwa ahadi hiyo.

“Tulivyoahidiwa na Mhe Rais tuliandaa kazi zetu vizuri tukiwa naimani kuwa zitashughuliwa na kuleta tija kama yalivyo makusudio yetu lakini tumekwama nazo tunamkubushia mama yetu Mpendwa atukumbuke na kuelekeza kwa wasaidizi wake kupitia wizara husika watusaidie kama alivyotuahidi make ni muda sasa umepita hatujapata mrejesho wenye matumaini” wameeleza wawili hao.

Katika hatua nyingine wamebainisha kwamba wamekuwa wakizipitia changamoto mbalimbali wanapokuwa na kazi zao na kutaka kuzitengeneza kwenye studio za watu wakati wimwingine hushindwa kufanya hivyo kutokana na uhaba wa kifedha za kuwawezesha malipo kwa wenye studio jambo ambalo limekuwa kikwazo kikubwa chakuwakwamisha na kushindwa kupiga hatua ya kusonga mbele kupitia sanaa yao ya kuimba na kughani.

Wamefafanua kwamba nyimbo zao na mashairi hayo pakubwa yamejikita kutangaza mambo mengi na makubwa kimaendeleo yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivyo wamesisiza kuwa iwapo watafanikiwa ahadi hiyo wanamatumaini makubwa yakwamba ujumbe wao utawafikia watanzani wengi hapa nchini.

Hata hivyo wamewaomba viongozi wa Serikali ya Mkoa Kagera kuwatambua vyema kwakuwapa kipaumbele wao na kazi zao hizo kwakuwashirikisha katika majukwaa mbalimbali ya mikutano yanapokuwa yametokea ili nao waonyeshe ujuzi wao kwa jamii kama ilivyo kwa wasanii wengine wasio walemavu.

“Sisi kwenye mikusanyiko ya mikutano hasa ya viongozi muda mwingi huwa tunajipeleka ukifika wakati mwingine utaulizwa umeitwa? kweli hii siyo nzuri sisi ndiyo niwatu wenye ulemavu lakini tuna mambo makubwa yakufanya kama wale wasio walemavu tuungeni mkono na sisi tujenge Mkoa wetu na nchi yetu kwa nguvu moja” wameendelea kubainisha kwa undani.

Wamehitisha wakitoa pongezi kede kede kwa Serikali natimu nzima ya viongozi wakitaifa wakiongozwa na Rais Samia kwa jinsi inavyoendelea kuchapa kazi thabiti na kwa umakini mkubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo zaidi huku wakishukuru wanavyotambuliwa nakuthaminiwa kwa sasa watu wenye ulemavu kote nchini hivyo wameomba wadau kujitokeza nakuwashika mkono ikiwaweza kutengeneza kazi zao ambapo wametoa mawasiliano yao kuwapata kwa ukarbu kwa mtu mwenye kuwiwa nakuwasaidia 0742346809 na 0767544745.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!