Home Kitaifa WAKAZI KATA YA MCHIKICHINI WAFUTWA MACHOZI BAADA YA KILIO CHA MUDA MREFU

WAKAZI KATA YA MCHIKICHINI WAFUTWA MACHOZI BAADA YA KILIO CHA MUDA MREFU

Na Magreth Mbinga

Wananchi wa Kata ya Mchikichini,Wilaya ya Ilala wametakiwa kujivunia mradi wa kituo cha afya ambao anatarajiwa kuanza ujenzi hivi karibuni katika Kata hiyo ambao unajengwa kutokana na mapato ya ndani ya Nchi yanayotokana na ukusanyaji wa kodi mbalimbali utakaoghalimu shilingi Bilioni 500 na Milioni 300.

Hayo yamesemwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mh.Mussa Azzan Zungu akiwa mgeni rasmi katika hafla ya utiaji wa saini wa ujenzi wa mradi huo katika eneo ambapo mradi utatekelezwa mchikichini Ilala Jijini Dar es Salaam.

“Tunafanya haya kwa sababu yenu tunajenga kituo hiki kwa fedha za ndani tumuunge mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia kulipa kodi ukinunua dai risiti na ukiuza toa risiti tulipe kodi tijenge Taifa letu wenyewe” amesema Mh Zungu.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Ng’wilabuzu Ludigija amesema ujenzi wa kituo hiko cha afya kitakuwa kituo cha nane kujengwa katika Wilaya ya Ilala katika kipindi kifupi sana na kuna vituo vingine vinaendelea na ujenzi vikiwa katika hatua mbalimbali kuna kituo kinajengwa Segerea ,Kinyerezi,Kiwalani,Zingiziwa,Majoe, Kipunguni,Mwanagati na Kata ya Mzinga .

“Hii yote ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi na Mama Samia anatekeleza kwa kutoa huduma muhimu hasa ya matibabu tunamshukuru sana sisi kama Wilaya ya Ilala kwa upendeleo mkubwa ambao ameendelea kutupatia” amesema Dc Ludigija.

Aidha Mstahiki Meya wa Jiji la Ilala Mh Omary Kumbilamoto amewataka wananchi kusimamia mradi wao wenyewe kwani jukumu la kusimamia mradi huo sio la Mkuu wa Wilaya wala Mbunge kwasababu ni fedha ambazo Mh Rais amewapatia kwaajili ya kukomboa Kata ya Mchikichini.

“Ninamatumaini Kata za jilani za Wilaya ya Ilala ambazo hazina zahanati kama Kariakoo hakuna kituo cha afya wala zahanati,Kata ya Buguruni hakuna kituo cha afya wala zahanati tunaona mtu akipata homa mpaka aende hospitali binafsi” amesema Mh Kumbilamoto.

Sanjari na hayo Mh Kumbilamoto amesema kituo hiko kikubwa cha afya kitakacho kuwa na ghoro nne kitakusanya mapato mengi katika Wilaya hiyo na kutakuwa na huduma ya bima ya afya ambapo ukombozi mkubwa sana utapatikana kwa wakazi wa Kata hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!