Home Biashara WADAU WA SEKTA MBALIMBALI WAMEKUTANA NA BRELA ILI KUREKEBISHA SHERIA YA LESENI

WADAU WA SEKTA MBALIMBALI WAMEKUTANA NA BRELA ILI KUREKEBISHA SHERIA YA LESENI

Na Magreth Mbinga

Sheria za biashara hazitakiwa kuwa mgando zinatakiwa ziendane na mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa kama hali inavyoendelea Duniani na Nchini.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara BRELA Ndugu Andrew Mkapa katika ufunguzi wa kikao cha kukusanya maoni ya wadau kuhusu marekebisho ya sheria ya leseni za biashara sura 208.

“BRELA ikiwa ni mmpjawapo ya mamlaka inayotoa leseni za biashara ifanya mchakato wa kuwasiliana na Wizara mama ambayo ni Wizara ya Uwekezaji ,Viwanda na Biashara Waziri wake ndio mwenye dhamana ya kusimamia sheria hii kwaajili ya kupendekeza kufanya marekebisho mbalimbali ya sheria hii ili iweze kuendana na wakati na mabadiliko yaliyotokea”amesema Ndugu Mkapa.

Pia amesema Wizara ya Uwekezaji Viwanda na biashara iliunda kikosi kazi ambacho kilikaa na kufanya mapendekezo ya awali ya marekebisho au maboresho ya sheria hiyo na baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo kwa Waziri mwenye dhamana ya maswala ya biashara na akaagiza kutaka kuonana na wadau ili aweze kupata maoni ya wadau ambao ndio wanaotumia hiyo sheria.

Aidha Mkapa amesema kikao hiko kitakuwa cha siku tatu ambapo wamepanga makundi siku ya kwanza watakutana na wadau wa Taasisi za Serikali,siku ya pili watakutana na wadau wa Sekta binafsi na siku ya mwisho kikosi kazi kitafanya majumuisho yote na kuyapeleka kwa Waziri mwenye dhamana ya sheria hiyo.

“Sheria hii inavipengele zaidi ya thelasini miaka ambayo sheria inaundwa hakukuwa na biashara za mtandao lakini kwa mabadiliko ya teknolojia na ufanyaji biashara sasahivi sasahivi zimeingia biashara za mtandao zinakuwa hazijajumuishwa kwenye leseni”amesema Mkapa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!