Home Kitaifa TIGO YASHIRIKIANA NA BOOMPLAY KUIMARISHA USIKILIZAJI WA MUZIKI KIDIJITALI TANZANIA

TIGO YASHIRIKIANA NA BOOMPLAY KUIMARISHA USIKILIZAJI WA MUZIKI KIDIJITALI TANZANIA

Kampuni inayoongoza kwa huduma za mawasiliano nchini Tanzania, Tigo, leo imetia saini na kutangaza ushirikiano wa kimkakati na App namba moja barani Afrika, Boomplay, utakaowawezesha wateja wa Tigo kupata unafuu wa gharama na kusikiliza muziki bure kupitia App ya Boomplay kama sehemu ya Kampeni ya Wakishua.

Kampeni ya Wakishua inadhihirisha dhamira ya Tigo katika kuboresha mageuzi ya kidijitali kwa wateja kote nchini huku ikitafakari kuhusu mabadiliko ya chapa kwa wakati.

Wateja wa Tigo nchini Tanzania kuanzia sasa, mara baada ya kujiunga na vifurushi vya siku, wiki au mwezi watasikiliza muziki bure kupitia App ya Boomplay. Sambamba na hilo, wateja wa Tigo watafurahia punguzo la asilimia 30 watakapohitaji kujiunga na malipo ya  siku, wiki au mwezi ya Boomplay.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tigo, William Mpinga alisema, "Mtandao wa Tigo umekuwa ukisaidia tasnia ya muziki kwa muda sasa kwa kutoa fursa kwa wasanii kuungana na mashabiki zao, hivyo tuna furaha kutoa jukwaa litakalo endeleza dhumuni hili. Tunatambua hitaji la wateja nchini Tanzania kuwa na chaguzi zaidi za kupata muziki na burudani, na kukidhi hitaji hili; hakuna mtoa huduma bora wa kushirikiana nae zaidi ya Boomplay. Kupitia uzinduzi wa kampeni hii ya Wakishua, tunawapa wateja wetu jukwaa la kidijitali ili kusikiliza bila malipo, ubora wa sauti na machaguo mapya ya muziki.

Pia akizungumzia ushirikiano huo, Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli, alisema, “Maono yetu ni kuwezesha sekta ya muziki wa Kiafrika na kuhakikisha unafika mahala pazuri, hivyo, tuna matumaini makubwa kupitia ushirikiano huu na Tigo. Tunaamini ushirikiano wetu utaongeza usikilizwaji wa nyimbo zaidi ya milioni 85 kwenye App ya Boomplay na kuongeza kipato kwa wasanii wa Tanzania katika siku za usoniā€.

Kampeni ya Wakishua inaruhusu wapenzi wa muziki kuwasikiliza wasanii wanaowapenda wa ndani na nje ya Tanzania kwa kutumia fursa ya ofa ya usikilizaji muziki bila malipo kupitia Boomplay na hatimaye kuongeza kipato kwa wasanii hao.

Wateja sasa wanaweza kufurahia machaguo mbalimbali ya muziki kwenye App ya Boomplay kwa kununua kifurushi chochote kutoka Tigo. Kwa wale ambao bado hawapo kwenye mtandao wa Tigo, wanaweza kupata SIM kadi ya Tigo kote nchini na kupakua App ya Boomplay na kuwa sehemu ya kundi la Wakishua.

Watumiaji wa Boomplay kupitia mtandao wa tigo wanahimizwa kusasisha programu yao ya Boomplay hadi toleo jipya zaidi ili kufurahia vipengele na matoleo mapya. Ofa ya Wakishua inapatikana tu kwenye toleo la programu ya Boomplay v6.1.20 na matoleo mapya zaidi kwenye Android na v4.4.0 na matoleo mapya zaidi kwenye iOS.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!