Home Kitaifa TIC YAELEZA SABABU ZA USHIRIKI MAONYESHO YA UWEKEZAJI SABASABA

TIC YAELEZA SABABU ZA USHIRIKI MAONYESHO YA UWEKEZAJI SABASABA

Na; Theresia Allan
Taasisi inayohusika kuweka mazingira Bora ya uwekezaji nchini Tanzania (TIC) imetangaza fursa za vipaumbele dhidi ya uwekezaji nchini katika maonyesho ya 46 Saba Saba.


Akizungumza katika maonyesho hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TIC Ndugu John Mathew Mnali kuhusu huduma za uwekezaji zinazotolewa kwenye jamii na taasisi hiyo pamoja na fursa zilizopo, amesema kuwa huduma hizi zimewekwa Kwa mpangilio maalum ili kuwezesha kutoa huduma stahiki Kwa wawekezaji pamoja na wananchi kwa lengo la kutoa elimu Kwa wananchi wenye nia ya kuwekeza.


Pia amewataka wananchi ambao hawakuweza kufika kutembelea vituo vya uwekezaji vilivyopo karibu yao kwenye ofisi za kanda ili kupata huduma zinazotolewa kwa ajili yao.

Tunapenda kuwajulisha Wananchi ambao hawakupata Fursa ya kuja kwenye maonesho haya, Kituo Cha Uwekezajikina ofisi kwenye kanda; kaskazini kipo kwenye majengo ya Ofisi za Mkuu wa Mkoa, nyanda za juu kusini zipo kwenye Jengo la NBC Mbeya na Kanda ya ziwa zipo Barabara ya Uhuru mkabala na jengo la NSSF na nyingine ipo Dodoma jengo la zamani lililokuwa likutumika na halmashauri ya jiji Dodoma” – Mnali

Ushiriki wetu Kwa mwaka huu umekuwa tofauti kidogo, kwanza mwaka huu tumebebwa na kauli mbiu ya “TANZANIA NI MAHALI SAHIHI KWA BIASHARA NA UWEKEZAJI” na kama mnavyofahamu kituo Cha uwekezaji kina jukumu kubwa la kuhamasisha uwekezaji wa ndani na nje” alisisitiza hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC

Aidha amewataka wananchi kujitokeza na miradi yao ili iweze kupata vivutio vya uwekezaji Kwa kupata cheti kitakacho punguza gharama za uwekezaji.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!