Home Kitaifa TBS WATOA ELIMU YA VIWANGO, MAONESHO YA 12 YA BIASHARA KIMATAIFA ZANZIBAR

TBS WATOA ELIMU YA VIWANGO, MAONESHO YA 12 YA BIASHARA KIMATAIFA ZANZIBAR

 Na Mwandishi Wetu.

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya viwango kwa wananchi na wajasiriamali wanaotembelea Maonesho ya 12 ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Dimani.

Akizungumza katika maonesho hayo, Afisa Uhusiano wa TBS, Bi. Gloria Mgomberi, amesema lengo la utoaji wa elimu hiyo ni kuongeza uelewa kwa wananchi ili waweze kuzingatia masuala ya viwango kwenye bidhaa zinazouzwa sokoni.

Ameeleza kuwa wananchi wanaotembelea banda la TBS katika maonesho hayo wanapatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kuzingatia viwango vya bidhaa pamoja na kusoma taarifa zilizopo kwenye vifungashio kabla ya kununua bidhaa.

Bi. Gloria amesisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kulinda afya na usalama wa watumiaji pamoja na kudhibiti bidhaa zisizokidhi viwango kuingia sokoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!