Shirika la TADEPA ambalo si la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kijamii hususani kwa upande wa watoto lenye makao yake makuu Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera limeshauri kuwa Serikali, wadau na jamii kwa ujumla kuongeza juhudi za kutenga rasilimali muhumu kwa ajili ya malezi na makuzi Bora ya mtoto.
Akitoa ushauri huo Afisa mradi jumuishi wa malezi na maendeleo ya awali ya mtoto (NMECDP) Abimeleck Richard unaojumuisha wadau mbalimbali unaotekelezwa Mkoani Kagera amesema kwamba ili mtoto aweze kufanikiwa kukua kwa maendeleo mazuri ni vyema bidii ikawepo ya kuwekeza kwa watoto kuanzaia umri wa chini ya miaka 10 hadi 8.

Ameyazungumza hayo mbele ya waandishi wa habari katika kikao kilichoandaliwa na shirika hilo Manispaa ya Bukoba kwa ajili ya kukutana na baadhi ya waandishi wa habari juu ya kuwaelimisha namna ya kuifikia jamii kwa usahihi hususani katika kuineza programu hiyo ya jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwani vyombo vya habari vina nafasi kubwa mno ya kuifikia jamii katika kuhabarisha umma mambo mbalimbali hatimaye kuleta matokeo chanya katika utatuzi wa changamoto za wananchi.
“Ndugu zangu ni wambieni ukisha wekeza kwa watoto hawa maanake unatarajia kupata mafanikio makubwa ndo maana programu hii jumuishi ina wizara mbalimbali zinazoingiliana ambazo ni wizara ya Afya, wizara ya Elimu wizara ya maendeleo ya jamii yaani idara yoyote inayohusika na mtoto inahusika katika mpango huu kwahiyo mpango huu siyo wa mtu mmoja ni wakila mmoja kushiriki kwa namna moja au nyingine ndo maana hata nyie waandishi wa habari tumewajumuisha kwa umuhimu sana lakini lengo ni kumfanya mtoto mdogo tuwekeze rasilimali zinazohijika kwake ili tuwezeshe mazingira yake ya kujifunzia, au kama ni kliniki vituo vya afya na kadharika lakini lengo lake zaidi ni kwamba baadaye awe ni mtu mwenye kutumainiwa katika ujenzi wa Taifa” amefafanua Afisa Mradi Abimeleck Richard.
Rasilimali hizo zinahusisha kwenye lishe bora, afya, ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama wa mtoto vipengere vyote hivi ndivyo vinavyomfanya mtoto wa mwaka 0 hadi 8 aweze kukua katika mazingira wezeshi na ya kuvutia kwake bila kufanya hivyo matokeo yake tunaona baadhi ya watoto wamekuwa wakiishi wakikabiliwa na changamoto mara kadhaa katika mazingira tofauti tofauti kuanzia kwenye familia zao hata shuleni mfano kule shuleni utakuta madarasa ya kuanzia darasa la saba la nne ndo yamewekwa kwenye kipaumbele zaidi kwa sababu ya mitihani lakini darasa la awali ambako wanajifunzia watoto wale wadogo sana wao wanachukuliwa kawaida na darasa lao utakuta limetengwa huo kabisa jambo ambalo si rafiki sana katika kumchipua mtoto kwenye misingi yenye ubora unaohitajika kwa mtoto kwahiyo ni vyema tukawekeza nguvu zaidi katika kuwalea watoto hawa maana msingi wa kukua kwa binadamu ni darasa la awali hapo ndo kitovu cha ubora wa makuzi ya mtoto” amehitimisha Afisa Abimeleck Richadi.

Agnes Joseph ambaye ni Afisa utawala wa shirika hilo naye ameigusia suala la madara ya watoto wa awali kuwa zinahitajika jitihada thabiti katika ukuaji wa watoto make muda mwingi watu hudili na madara ya juu kuliko madara ya watoto hao mengi hujikuta yakiwa chakavu kuliko madarasa ya juu hivyo yapaswa kuongeza uboreshaji katika eneo hilo ili kuwapatia elimu iliyo bora.

Naye Dr. Jems Barongo Mkurugenzi wa TADEPA amesisitiza kwenye eneo la kutenga rasilimali za vyakula bora kwa ajili ya lishe bora kwa watoto maana lishe bora ni chanzo muhimu katika makuzi ya watoto kuanzia mimba hata baada ya kuzaliwa.

Naye Mwandishi wa habari kinara wa bahari za programu hiyo Arbogast Mutayoba amesema kuwa programu hiyo ya jumuishi ya Taifa ilianza mwaka 2021, 2022 na inaendelea hadi mwaka 2025 na 2026 ikiwa na malengo ya kuhakikisha zinawekezwa rasilimali za kutosha hasa katika umri mdogo kuanzia mwaka 0 hadi miaka 8 na hiyo nikutokana na umri huo ubongo wa mtoto unajengeka katika kujua mambo mbalimbali ya kidunia vilevile nakulelewa katika misingi iliyo bora inayowafanya kuwa raia wema nawaweze kulitumia taifa kwa uzalendo na uaminifu.
Kepha Elias akishiriki kwenye kikao hicho akimwakilisha Afisa maendeleo ya jamii Mkoa amekili kuwepo kwa changamoto kadhaa kwa watoto hususani katika makuzi ambayo sirafiki kwa baadhi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya baadhi ya wazazi kutokutilia maanani suala zima la malezi bora ya mtoto hasa kwa upande wa kutimiza wajibu wakuwapatia lishe bora ukizingatia hali ya takwimu za lishe kwa Mkoa Kagera kutokuwa katika kiwango kizuri hivyo ameahidi kuwa Serikali ya Mkoa iko tayari kutoa ushirikiano utakaokuwa ukihitajika katika utekelezaji wa mradi huo kwani ni muhimu sana katika kuinua kiwango cha juu cha maelezi bora kwa watoto Mkoani humo.








