Home Kitaifa TAASISI YA ECKERNFORD YAWASHAURI VIJANA, SERIKALI KUCHUKUA HATUA HIZI ILI KUENDANA NA...

TAASISI YA ECKERNFORD YAWASHAURI VIJANA, SERIKALI KUCHUKUA HATUA HIZI ILI KUENDANA NA SOKO LA AJIRA NCHINI

Na. BONIFACE GIDEON, TANGA

Taasisi ya Elimu Jijini Tanga ya Eckernford ( Eckernford Institute of Education) imewashauri Vijana wanaohitaji kujiari na wale wanaotafuta Ajira wachukue Kozi ambazo kwa sasa zinaendana na Soko la Ajira hususani za Ufundi mbalimbali ikiwamo ufundi wa kushona nguo, Magari, Uchomeleaji, Udereva.

Ushauri huo umetolewa leo na Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Mohammed Satindi aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya namna Vijana wanavyoweza kuchukua hatua ili kujikwamua na tatizo la Ajira hapa nchini kwa kujiari au kuajiriwa kwa haraka.

Satindi Alisema Endapo Vijana Wataamka na kujiunga kwenye vyuo vya Ufundi tatizo la Ajira nchini litapungua kwa kiwango cha hali ya juu kwakuwa kozi za Ufundi humfundisha Mwanafunzi kwa Vitendo zaidi na Mwanafunzi Baada ya kumaliza hupata fursa ya kuchagua Kati ya kuajiriwa au kuajiriwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!