Home Kitaifa TAASISI YA BILAL MUSLIM YAWAFUNDA WAZAZI MALEZI MAZURI YA WATOTO KATIKA MISINGI...

TAASISI YA BILAL MUSLIM YAWAFUNDA WAZAZI MALEZI MAZURI YA WATOTO KATIKA MISINGI YA KIDINI

NA BONIFACE GIDEON, TANGA

Wito umetolewa kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini kuhakikisha wanawalea Watoto katika Maadili Mema ya Kidini ili kujenga Taifa la Watu Wema na Wenye hofu ya Mungu.

Wito huo umetolewa Mwishoni mwa Wiki na Mkuu wa chuo Kikuu wa Kidini Cha Bilal Muslim Mission Tawi la Tanga Sheikh Kadhim Abbas Wakati wa mahafali ya 11 ya kuhitimu Shahada ya Elimu ya Dini katika Chuo kikuu Cha Kidini Cha Bilal Muslim Mission Tawi la Tanga kilichopo Barabara ya Nne Tanga Mjini.

Katika Mahafali hayo Jumla ya Wanachuo 14 wa Elimu ya juu ya dini ya Kiislamu Walitunukiwa shahada kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Bilal Muslim Mission Tawi la Tanga kati yao Wanaume 9 na Wanawake 5 .

Sheikh Kadhim Abbas alibainisha kwamba Elimu ya Dini ya Kiislamu imeweka milango wazi kwa mtu yeyote kujiendeleza kwa kadri anavyohitaji na kwamba Elimu ya Dini Haina Mipaka ya Umri

Aliongeza kuwa Elimu ya Dini imesisitizwa katika maandiko matakatifu ya Mtume Mohamed (SWA) akiwasisitiza maswahaba umuhimu wa kuitafuta elimu,

Ndugu zangu katika Uislamu mliohitimu elimu ya Chuo kikuu, leo mnaingia katika maisha mapya ya kumfuata Mtume wetu Mtukufu kwa
kuvikwa kilemba, ishara kwamba ninyi sasa ni Maulamaa”.
alisema

Alisisitiza kwamba Uislamu ni dini moja ingawa ina madhehebu mengi,
lakini msingi wao mkubwa ni katika kumwabudu Mwenyezi Mungu na Kuifanya Jamii kuishi Maisha yanayompendeza Mungu pamoja na Jamii kwa Ujumla.

Naye Sheikh Hamis Awadh Mussa ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya Ndani na Nje alisema Chuo hicho ni moja ya vyuo vikuu vya kidini katika Taasisi hiyo ya Bilal Muslim Mission alisema kwamba wataendelea kuwasomesha vijana wengi zaidi ili kuongeza idadi ya waalimu katika vyuo mbalimbali nchini pamoja na misikiti

“Taasisi yetu inaendelea na utaratibu wa kuwajenga vijana katika misingi ya kidini, lakini pia wanapata elimu ya jumla inayosaidia
kuishi maisha ya kimaadili yanayompendeza Mwenyezi Mungu na jamii kwa ujumla.

Aidha alivitaja vyuo vikuu vingine vya kidini ambavyo vinamilikiwa na Taasisi hiyo hapa nchini kuwa ni pamoja na Tanga, Arusha, Dar es
Salaam,Mwanza, Dodoma, Kigoma, Bukoba na Moshi.Aliongeza kwamba kila mkoa kuna vyuo vidogo ambavyo vipo maalumu kwa ajili ya kuwajengea vijana maadili ya kidini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!