Home Kitaifa SERIKALI YAVITAKA VYUO KUWEKA MSISITIZO ZAIDI MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI

SERIKALI YAVITAKA VYUO KUWEKA MSISITIZO ZAIDI MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI

SERIKALI imevitaka vyuo kuzingatia mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi ili kuondoa malalamiko kutoka kwa waajiri kwamba wahitimu wengi wanahitimu bila kuwa na ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira.

Hayo yamesemwa leo tarehe 12 Novemba, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako Mb) alipomuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye mahafali ya 57 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salam ambapo wahitimu 1,065 walitunukiwa vyeti vya ngazi mbalimbali.

Mhe. Ndalichako Amesema kuwa mafunzo mengi kufanyika kwa madharia bila vitendo na amekipongeza chuo cha CBE kwa kuanzisha programu ya uanagenzi ambapo mwanafunzi anasoma nusu ya masomo chuoni na nusu akiwa sehemu ya kazi.

Ndiyo sababu naipongeza CBE kwa kuanzisha program ya uanagenzi ambayo mwanafunzi anakua darasani kwa asilimia 50 na anakuwa sehemu ya kazi kwa asilimia 50 na kwa kufanya hivi unatatua changamoto iliyokuwepo ya kuwa na wahitimu ambao hawana ujuzi sawasawa,” amesema Mhe. Ndalichako.

Alisema serikali katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 ilitenga Sh bilioni 9 ambazo ziliwezesha vijana zaidi ya 62,000 kupata mafunzo ya uanagenzi na katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 kwa ajili ya kuendelea kutoa mafunzo ya uanagenzi.

Mhe. Ndalichako Amepongeza Profesa Emmanuel Mjema kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa mkuu wa chuo hicho kwa kipindi cha miaka 10 kwani chini yake chuo kimepata mabadiliko makubwa kitaaluma kwani alikipokea kikiwa katika hali mbaya.

Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kujali maendeleo ya wananchi kwa kuhakikisha wanapata huduma stahiki kwa kuboresha huduma vyuoni.

Mhe. Kigahe amempongeze Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, ambaye ni mlezi wa Kampasi ya CBE kwa kukubali kutenga muda na kushiriki katika jitihada za kuchangisha fedha ili kusaidia kukamilisha ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike katika kampasi ya Mbeya.

Mhe. Kigahe amewakaribisha Viongozi na wadau mbalimbali kushiriki katika kongamano la kitaaluma la tatu linaloratibiwa CBE, lenye kaulimbiu “Biashara, Uwekezaji na Ubunifu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi”. Ambapo linatarajiwa kufanyika tarehe 15 na 16 Novemba, 2022 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!