Na Magrethy Katengu
Serikali imewataka wamiliki Wasimamizi, Mameneja na Walezi wa vituo vya kulelea Watoto chini ya umri wa miaka 5 (Day care) kuhakikisha wanasajili vituo vyao ili viweze kutambulika na yeyote atakayebainika anaendesha kituo pasipo usajili hatua kali itachukuliwa dhidi yake ikiwemo kufungiwa.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam wakati akifunga Mafunzo yaliyoendeshwa siku kumi kwa wamiliki, wasimamizi, mameneja na walezi wa vituo hivyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Wakili Amoni Mpanju amesema ifike mahali vituo visiendeshwe pasipokuwa na weledi na usalama wa Watoto hivyo lazima vituo vyote nchini vitambulike na kukaguliwa mara kwa mara na watoto wanaolelewa muongozo uliotolewa unafuatwa.
“Kuna Mtaala wa mafunzo ambao umeshaandaliwa na shule zitakapofungwa walezi,Wasimamizi ,mameneja wote wanatakiwa kuhudhuria ili waendelee kupata uzoefu kupitia mafunzo hayo kwani itawasaidia kulea Watoto vizuri kuepukana na Mmomonyoko wa maadili na kujenga Taifa lenye kizazi chema cha kesho” amesema Wakili Amoni
Hata hivyo Wakili Amoni amesema serikali kwa kushirikiana na wadau na mbalimbali ambao wameazisha vituo vya kulea Watoto mchana pamoja na vituo vya Watoto yatima kuhakikisha wanapata mafunzo bora ya maeneo yenye ulizi na usalama wa Watoto maswala ya ulezi wa Watoto kuhakikisha wanapata ujuzi.maarifa kwenye vituo wanapolelewa mchana kwakuwa walezi Wapo karibu nao wanaweza kutambua na kuibua vipaji vya Watoto hao tangu wakiwa wadogo .
Naye Kamishna Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Nandera Mhando amesema wepokea maagizo yote waliyopewa watahakikisha wanafuatilia na wanatekeleza ili kuleta jamii yenye maadili mema.
Aidha mafunzo hayo yanaendeshwa nchi nzima hivyo kwa mkoa wa Dar es salaam wilaya zilizonufaika ni Temeke, Ilala, Kigamboni, Kinondoni, na Ubungo hivyo mafunzo hayo yanatakiwa kutolewa nchi nzima kipindi cha likizo








